HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 21, 2022

Taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa tembo kata za Mkiwa na Misughaa wilayani Ikungi

 

 

Tumeendelea kupokea na kufuatilia mwenendo wa taarifa za uwepo wa TEMBO katika maeneo ya kata za Mkiwa na Misughaa wilaya ya Ikungi

Ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine wanaendelea kuwafuatilia Tembo wanaonekana katika makazi ya watu katika maeneo tajwa

Aidha ofisi ya wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine imefanya kikao kazi na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith S. Mahenge Jana Tarehe 20/06/2022 na kukubaliana kuchukua hatua zaidi za kudhibiti Tembo walioko kwenye makazi ya wananchi

Kwa Taarifa hii, tunaomba wananchi katika maeneo tajwa kuendelea kuchukua tahadhari ya usalama wao, pia tunaomba wananchi kuacha Tabia ya kuwashambulia, kuwakimbiza au kuwasongasonga Tembo wanaopita katika maeneo yao badala yake watoe taarifa kwa mamlaka husika za vitongoji, vijiji, kata na hata wilaya

Ofisi ya Mkuu wa wilaya Ikungi inapenda kuwahakikisha wananchi Serikali inafanya kila linalowezekana katika mamlaka zetu kuondoa changamoto kwa haraka.

 Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ikungi
 21/06/2022


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad