HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 17, 2022

Shule za Atlas kuagiza mabasi 40 kuboresha usafiri kwa wanafunzi

Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa akipanda mti mara baada ya kuzinduliwa Clabu ya Upandaji miti katika shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022.KATIKA kuboresha miundombinu ya usafiri katika shule za zinazomilikiwa Atlas Mark Group washirikiana na kampuni ya Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd ya nchini Japani wanatarajia kununua Magari 40 kwaajili ya kurahisisha usafiri katika shule hizo.

Akizungumza wakati walipotembelewa na Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz kutoka Japan jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa amesema kuwa kukamilika kwa ununuaji magari hayo kutaboresha suala la usafiri katika shule hizo.

"Katika kuboresha usafiri katika shule za Atlas tunaweka jitihada kwa kushirikiana na benki ya UBA na kutoka fedha za ndani tunataka angalau kwa miaka miwili kuanzia mwaka huu hadi Juni 2023 tunatarajia kuwa tumeingiza mabasi Mapya 40 na ambayo yametumika kwa miaka michache na mpaka sasa tunavyoongea 10 yapo kwenye maeneo ya kuhifadhia magari hapa nchini.

Na tayari Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd wa Japani ameruhusu yale magari mapya tuyatoe na tuanze kuyatumia wakati tunaendelea kuongea na benki na kuendelea kujenga uwezo wa ndani." Amesema Rugambwa

Amesema shule za Atlas zinahitaji usafiri kwa sababu kipindi fulani zimepitia matatizo ndani ya miaka mitatu iliyopita kiasi kwamba kushuka kwa Kipato.

Amesema kuwa ili kurudisha imani kwa wazazi na jamii nzima wameanzisha Suala za usafiri mzuri katika Shule mbili za Atlas zilizopo jiji la Dar es Salaam ili watoto waweze kuutumia wakiwa wanaenda shuleni.

Amesema kuwa benki yeyote itakayo shirikiana na shule hiyo wataweka matangazo ya benki hiyo ili kufanya shule nyingine waweze kuulizia fursa hiyo imetokana na nini?

"Hivyo tukishirikiana hivyo inaweza kusababisha mahusiano mazuri kati ya sisi shule, Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd kutoka Japani na benki tutakayokuwa kumeshirikiana." Amesema Rugambwa

Amesema kuwa wakati kipato cha shule kilivyokuwa kizuri walikuwa wanawanunulia magari walimu wa shule hizo, ingawa kwa sasa wafanyakazi wameomba kuletewa magari yao binafsi na kampuni hiyo ya Japani.

Amesema utaratibu ukikamilika mpaka kufikia mwakani wafanyakazi watakuwa tayari na uwezo wa kununua magari kutoka nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango, Fedha, Utawala na Sheria wa Atlas Mark Group, Didas Kanyambo amesema majadiliano ya leo ilikuwa ni kukuza mahusiano ya kibiashara kati ya Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd ya nchini Japani hasa ikilenga kwenye suala la uboreshaji wa huduma ya usafiri kwenye shule za Atlas jijini Dar Es Salaam.

"Amekuwa akituuzia magari takribani miaka mitano iliyopita lakini hadi sasa tunaompango wa kuweza kuingiza mabasi mengine 40." Amesema Kanyambo

Amesema magari hayo yataenda kwa awamu tofauti, ambapo kwa mazungumzo ya leo wamehakikishiwa kupata mabasi manne mpya kutoka kampuni hiyo ya Japani.

Amesema magari hayo yatatumika katika kuboresha usafiri huduma ya usafirishaji wa wanafunzi wa Shule za Atlas kwa usalama na kuwahi madarasani na kuweza kujifunza vile inavyostahili kwaajili ya mstakabali wa maisha yao na taifa kwa ujumla.

Kabla ya mazungumzo ya kuboresha usafiri shuleni hapo walipotembelewa na Ugeni kutoka Japani pia wslizindua Club ya upandaji Miti, Shirika lisilo la kiserikali la Sharon Ringo Foundation kwakupanda miti katika shule hiyo.

Pia walitembelea na kujionea majengo ya shule hiyo ikiwa pamoja na madarasa, mabweni, hospitali na maeneo mbalimbali ya kujifunzia.
Uongozi wa Shule za Atlas wakiwa na Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz kutoka Japan jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022  wakitembelea maeneo mbalimbali ya shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaaam.
Mkurugenzi wa Mipango, Fedha, Utawala na Sheria wa Atlas Mark Group, Didas Kanyambo  akitoa maelekezo wakati uongozi w shule na mgeni wa Kutoka Jampani alipotembelea katika shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz kutoka Japan akizungumza wakati alipofika katika shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022 
Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz akipanda mti mara baada ya kuzinduliwa Clabu ya Upandaji miti katika shule ya Atlas Madale jijini Dar es Salaam leo Juni 16, 2022.
Viongozi wa shule ya Atlas wakiwa katika picha ya pamoja.
Viongozi na Wafanyakazi wa shule ya Atlas wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz.
Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa akimkabidhi zawadi Rais wa Kampuni ya Goldenmiles co.Ltd, Syed Mahfuz mara baada ya kutembelea shule ya Atlas Madale na kufanya mazungumzo ya mahusiano ya kibiasha kwaajili ya kuboresha sekta ya usafiri katika shule hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad