HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 8, 2022

SERIKALI YADHAMIRIA KUTATUA KERO ZA WATUMISHI MZINGA

Mawaziri wakipata maelezo mara baada ya kufika Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro.
 waziri mhagama akiongea na wafanyakazi Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro wakati wa ziara katika shirika hilo ikiwa ni maatokeo ya ombi la Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na JKT, la kuwatembelea watumishi hao kwa lengo la kujionea kero zao na kutafuta namna ya kuzitatua.
Mawaziri walipowasili Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro.
SERIKALI imedhamiria kwa dhati kutatua changamoto za watumishi wa umma katika Shirika la Mzinga lililopo mkoani Morogoro ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb) aliyefanya ziara ya kutembelea Shirika hilo, akiwa ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Stergomena Lawrence Tax (Mb), kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa pamoja na kujua kero zinazowakabili Watumishi wa Umma.

Ziara hiyo ni maatokeo ya ombi la Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na JKT, la kuwatembelea watumishi hao kwa lengo la kujionea kero zao na kutafuta namna ya kuzitatua.

Akiongea na na Watumishi wa Shirika la Mzinga, Mheshimiwa Mhagama amesema kuwa ameamua kuja Mzinga kuangalia ustawi wa wafanyakazi na kuja kwake kumemwezesha kujionea kwa macho na kujifunza kuwa kuna jambo kubwa la kitaifa linafanyika kwenye Shirika hilo la la kipekee kwani linazalisha mazao ya msingi hapa nchini. Kwa maana hiyo, Serikali inatakiwa kuwekeza kwa watumishi hao.

Kuhusu changamoto za watumishi, akiwa Waziri wa utumshi na utawala bora Waziri Mhagama ameahidi kuzishughulikia changamoto zote zilizowasilishwa kwake na Meneja Mkuu wa Shirika. Aidha, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wao pasipo kusukumwa na kuambukiza spirit hiyo kwa taasisi zingine. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tuanaendana na maono ya Mheshimiwa Rais kuhusu ustawi wa wafanyakazi aliyoyatoa wakati anahutubia Bunge kwa mara ya kwanza. Katika eneo la watumishi wa umma watumishi Mheshimiwa Rais alibainisha mambo makuu matatu ambayo ni haki kwa watumishi wa umma, stahiki za watumishi wa umma na uwajibikaji kwa watumishi wenye kuleta tija.

Akitoa shukrani kwa Mheshimiwa Mhagama, Mheshimiwa Stergomena amempongeza kwa kutenga muda wake na kuja kuongea na watumishi hao licha ya majukumu mengine ya kitaifa aliyonayo.

Aidha, alibainisha kuwa maagizo aliyoyatoa Mheshimiwa Mhagama yana pande kuu mbili upande wa Wizara yake (Utumishi na Utawala Bora) na upande mwingine ni wa Wizara ya ulinzi na JKT, hivyo basi maagizo hayo hayana budi kufanyiwa kazi kwa pmoja na pande zote. Aidha, aliwasihi watumishi hao kuendelea kuwa wavumilia na kuchapa kazi kwa bidii wakati changamoto zao zikishughulikiwa.

Akiongea kuhusu kero za kiutumishi zinazowakabili watumishi hao wa umma Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Seif Hamis amezibainisha kuwa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa rasilimaliwatu, ukosefu wa motisha kwa watumishi, ukosefu wa posho ya mazingira hatarishi na malimbikizo ya madeni ya mishahara.

Hii ni ziara ya pili kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ambapo kwa mara ya kwanza alitembelea Shirika la Mzinga tarehe 05 Mei,2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad