HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 3, 2022

NEMC YAKUTANA NA MAAFISA MAZINGIRA NCHI NZIMA YASISITIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

  Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Kanda ya kati, Dk.Franklin Rwezimula,akizungumza wakati wa warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.Baadhi ya Maafisa Mazingira wakifatilia mada  wakati wa warsha ya maafisa mazingira wa mikoa, wilaya na Halmashauri zote nchini wenye lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira duniani kitakachofanyika Juni 5, Mwaka huu jijini Dodoma.

Na Janeth Raphael-DODOMA
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka Maafisa Mazingira nchini kutunza na kuhifadhi nyanzo vya maji lengo likiwa ni kutunza mazingira kwa vitendo.

Akiwasilisha mada leo Juni 6,2022 jijini Dodoma wakati wa warsha ya Maafisa Mazingira  wa Mikoa,Wilaya na Halmashauri zote nchini ,Meneja wa NEMC, Kanda ya Kati, Dk.Franklin Rwezimula, amesema kuwa maeneo mengi ya vyanzo vya maji nchini yamekumbwa na tatizo la uvamizi wa wafugaji na wakulima wakitafuta maji kwa ajili ya kunywesha mifugo na kilimo.

Dk.Rwezimula, amesema katika warsha hiyo watajadiliana mambo mbalimbali ikiwemo Sera ya Mazingira ya mwaka 2021 ambapo NEMC  watawasilisha mada mbalimbali.

'Licha ya kuwapo na Sheria za usimamizi wa vyanzo vya maji (Bahari, Maziwa, Mito, Mabwawa na Chemichemi), kumekuwapo na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za binadamu zinazofanyika bila kuzingatia Sheria zinazosimamia mazingira na rasilimali maji.'

Amesema kuwa  NEMC pamoja na Maofisa hao wamejipanga kwenye utekelezaji wa majukumu yao kusimamia Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021.

“Tutakuwa na mada za kuwasilisha ikiwemo uharibifu na utunzaji wa vyanzo vya maji ambapo ni utekelezaji wa Dera za Mazingira pamoja  na Sheria  ya Mazingira ya mwaka 2014 lakini ni utekelezaji wa maagizo aliyotoa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango  wakati anazindua sera ya Mazingira tarehe  12 mwezi wa pili,”amesema

Amesema NEMC wamejiandaa  na baadae kupitia kikao hicho watatoka na mkakati wa pamoja ya jinsi ya kutunza mazingira kwani utunzaji wa vyanzo vya maji ni muhimu.

“Vyanzo vya maji  vina umuhimu mkubwa mojawapo ni katika  umeme na matumizi ya nyumbani na kilimo pamoja na  mashambani, bila maji hakuna maendeleo ili tuwe na maendeleo  endelevu ni lazima tuwe na maji safi na salama,”amesema.

Hata hivyo amewakaribisha wakazi wa Dodoma kufika katika banda la NEMC lilopo katika viwanja wa Jakaya Kikwete ambapo hapo watapatiwa elimu jinsi ya kutunza mazingira.

Naye, Ofisa Mazingira kutoka Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Bakari Bakari, amesema kuwa wapo tayari kuhakikisha mazingira na vyanzo vya maji vinatunzwa kwa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.

“Kwani mazingira ni jambo mtambuka.Tupo bega kwa bega kuhakikisha mazingira yanatunzwa kama Mkoa wa Kigoma ambao una  Wilaya 8 tupo bega kwa bega na  Rais Samia ikiwa ni kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad