HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

MTANZANIA AMILIKI KITUO CHA TotalEnergies KIGAMBONI

 


 
KAMPUNI kinara ya Mafuta nchini TotalEnergies imeendelea kuwafikia watanzania wenye malengo ya kumiliki vituo vya mafuta kwa kuzindua kituo kipya cha mafuta Kigamboni jijini Dar es Salaam, kituo hicho kinamilikiwa na kuendeshwa na mtanzania Mohammed Salehe Affif aliyenufaika kupitia programu ya umiliki na uendeshaji (DODO) huku ikielezwa kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania pamoja na kushirikiana nao katika uwekezaji wa sekta hiyo ili kujenga uchumi imara.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni James Mkumbo amesema kuwa programu ya DODO inayoendeshwa na kampuni ya TotalEnergies ya kushirikiana na wazawa imeleta kituo cha kwanza cha mafuta cha TotalEnergies Kigamboni na  kampuni  hiyo ambayo huduma zake zinafahamika kwa Umma kupitia ubora wake na viwango vya kimataifa.

'' Kwa niaba ya wananchi wa Kigamboni na Serikali kwa ujumla niwashukuru TotalEnergies kwa kuendelea kuwafikia watanzania kwa kiwango kikubwa cha umiliki wa vituo vya mafuta na kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi kupitia ubunifu, uwekezaji na ajira kupitia vituo hivi.'' Amesema.

Mkumbo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyopelekea mwekezaji huyo mzawa kufanya uwekezaji mkubwa utakaowanufaisha wananchi wa Kigamboni kwa kupata huduma na kutoa ajira kwa vijana wa maeneo jirani.

Aidha amempongeza Mohammed Afiff kwa kuwawezesha wananchi wa Kigamboni kiushi katika ndoto zao kwa kumiliki kituo kipya cha kisasa kitakachotoa huduma kwa wakazi wa kigamboni na maeneo ya karibu na kutoa ajira kwa vijana wa maeneo ya jirani.

Amesema hiyo ni fursa kwa wananchi na wafanyabiashara wa Kigamboni kupata huduma katika kituo hicho kwa kupata huduma za mafuta, kutengeneza magari yao pamoja na kupata mahitaji mbalimbali kupitia duka la Bonjour linalopatikana ndani ya kituo hicho kwa uhakika na usalama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Vituo vya Mafuta vya TotalEnergies Marieme Sav Saw amesema kuwa Wilaya ya Kigamboni imekuwa ikikuwa kwa kasi kutokana na juhudi za Serikali za kuweka miundombinu wezeshi ya kibiashara inayovutia uwekezaji ikiwemo daraja la Nyerere, ujenzi wa barabara kutoka Ferry, Kibada na Kibada hadi Mwasonga hali iliyopelekea mzawa huyo kuwekeza kwa manufaa ya wanakigamboni na watanzania kwa ujumla.

Marieme amesema kuwa mahusiano hayo ni hatua kubwa katika kuendeleza soko la mafuta nchini na ni fursa kwa watanzania wenye maeneo na ndoto ya kumiliki vituo vya mafuta kuitumia program ya DODO yenye uhakika wa soko, mapato pamoja utambuzi kupitia chapa (brand,) ya TotalEnergies yenye kutoa huduma bora na salama ikiwemo za mafuta bora (excellium fuel) na vilainishi.

Pia amesema kuwa ni fahari kwa TotalEnergies kufanya kazi na Mohammed Afiff na wanawashukuru wateja wao kwa kuendelea kuwaamini na subira yavuta heri kwa sasa wakazi wa Kigamboni watafurahia huduma zenye ubora na viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake mmiliki na mwendeshaji wa kituo hicho Mohammed Afiff  amesema, amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na kampuni ya TotalEnergies kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa na ubia huo wa kufanikisha uzinduzi wa kituo hicho utanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo kwa huduma za mafuta na vilainishi, bidhaa kupitia duka la Bonjour pamoja na ajira kwa wakazi wa maeneo hayo.


Awali Meneja wa kuendeleza biashara kwenye vituo Thomas Meitaroni amesema, kituo hicho kinachomilikiwa na mtanzania ni matokeo ya programu ya umiliki na uendeshaji Dealer Owns, Dealer Operate, (DODO) programu iliyobuniwa mahususi kwa wawekezaji wenye maeneo ya kujenga vituo vya mafuta vyenye leseni halali zilizotolewa na mamlaka ya Tanzania kuingia ubia na na kutumia chapa (brand) ya TotalEnergies.

Amesema kupitia DODO wawekezaji wananufaika na kutumia nembo ya TotalEnergies kampuni namba moja ya uuzaji mafuta na vilainishi nchini, soko la uhakika kote nchini ambako vituo hivyo vimesambaa.

Uzinduzi wa  kituo hicho uliambatana na ofa maalum ambapo wateja walipata zawadi mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata punguzo la shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta waliyonunua.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni James Mkumbo akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hich na kueleza  kuwa programu ya DODO inayoendeshwa na kampuni ya TotalEnergies ya kushirikiana na wazawa imeleta kituo cha kwanza cha mafuta cha TotalEnergies Kigamboni na  kampuni  hiyo ambayo huduma zake zinafahamika kwa Umma kupitia ubora wake na viwango vya kimataifa. Leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni James Mkumbo akijaza mafuta kwenye gari ya mmoja wa wateja waliofika kupata huduma katika kituo hicho.
Mkurugenzi wa Biashara wa Vituo vya Mafuta vya TotalEnergies Marieme Sav Saw akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho na kueleza kuwa Wilaya ya Kigamboni imekuwa ikikuwa kwa kasi kutokana na juhudi za Serikali za kuweka miundombinu wezeshi ya kibiashara inayovutia uwekezaji. Leo jijini Dar es Salaam. 

 Mmiliki na mwendeshaji wa kituo cha TotalEnergies Kigamboni  Mohammed Afiff  akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho na kueleza kuwa amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na kampuni ya TotalEnergies kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa na ubia huo wa kufanikisha uzinduzi wa kituo hicho utanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo kwa huduma za mafuta na vilainishi, bidhaa kupitia duka la Bonjour pamoja na ajira kwa wakazi wa maeneo hayo.







Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya ufunguzi wa kituo hicho.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad