HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 8, 2022

MKURUGNEZI NEMC AFUNGUKA SUALA LA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 Na Janeth Raphael_Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka ametaja mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Jijini Dodoma katika maonesho ya mazingira, Mkurugenzi huyo amesema hali ya mazingira nchini siyo nzuri hivyo wameweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi, kusimamia Sheria na Kanuni ikiwemo kuwapa adhabu kali wale wanaofanya vitendo vya uharibifu wa mazingira.

“Mkakati wa kuelimisha umma nia yetu wananchi kutii Sheria bila shuruti na hili linakuja kwa kutoa elimu mtu akikata miti ahakikishe anapanda miti, pia suala la taka ngumu na makelele imekuwa ni changamoto,”amesema.

Mkurugenzi huyo amesema sababu za uharibifu wa mazingira ni ongezeko la watu, misitu kuvamiwa na shughuli za binadamu kuendelea katika maeneo ya vyanzo vya maji.

“ Sehemu ya vyanzo vya maji vimevamiwa yale maeneo yaliyotengwa mita 60 wameshindwa kuyalinda na baadhi ya watu wanatumia kilimo cha umwagiliaji kutoka mtoni.Ukienda Kigoma,Katavi,Mtwara kuna shughuli kubwa za kibinadamu zinaendelea hali siyo nzuri kwa upande wa rasilimali za misitu.

“Kumekuwa na ongezeko la mimomonyoka ya udongo hivyo mito yetu kujaa udogo na katika milima ambayo ilikuwa ni hifadhi sehemu kubwa zimevamia Mbeya, Uruguru hata kule Usambaani maeneo makubwa yamevamiwa.Mvua zikinyesha hakuna utulivu wa maji hivyo kumekuwa na mafuriko,”amesema.

“Tumekuwa tukitoa elimu kwa viongozi wa dini na kwa wamiliki wa kumbi za starehe, maeneo mengine utupaji wa taka ngumu zote hizo ni changamoto,”amesema.

Mkurugenzi huyo amezitaja hatua ambazo wamechukua wakizichukua nipamoja na kuwapiga faini wale wenye makosa pamoja na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka,akielezea mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya Wiki ya Mazingira jijini Dodoma.
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakati wa maonesho ya wiki ya mazingira yaliyomalizika DodomaMkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuelezea mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya Wiki ya Mazingira jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad