MFUMO WA KIMTANDAO WACHANGIO ONGEZEKO LA USAJIRI WA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 30, 2022

MFUMO WA KIMTANDAO WACHANGIO ONGEZEKO LA USAJIRI WA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA


Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wakiwa katika picha ya pamoja  katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46  ya Sabasaba jijini Dar es Salaam MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesajili zaidi ya wafanyabiashara wa mbolea nchini zaidi ya 3800 na kufikia Mwisho wa Msimu wa kilimo wa mwaka huu wamesajili wafanyabiashara zaidi ya 2200.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Juni 30, 2022 katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 maarufu kama saba saba, Kaimu MenejaTehama na Takwimu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Salehe Kejo amesema kuwaongezeko la usajili wa wafanyabiashara umechangiwa zaidi na matumizi ya Tehama katika mamlaka hiyo.

Kejo amesema kuwa shughuli kubwa waliyoifanya katika Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni kuanzisha mfumo wa Kieletroniki au mfumo wa kimtandao wa mbolea uliorahisisha utoaji wa huduma kwa wateja.

"Wateja ambao waliokuwa wakitoka mikoa mbalimbali kuja Makao Makuu ya TFRA kufatilia Leseni zao, vibali ya kuingiza na kutoa mbolea sasa hivi wanapata huduma hizo kwa njia ya kimtandao." Amesema Kejo

Amesema Mfumo wa TFRA unamgusa moja kwa moja mteja kwani utoaji huduma umeimarika kutoka mteja kupata leseni kuanzia siku ya tatu hadi wiki, kwa sasa Mtu anapata Leseni ile ile ndani ya lisaa limoja tu.

Huduma nyingine zinazopatikana kwa haraka na kwa muda mchache ukilinganisha na muda wa kabla ya Mfumo wa kimtandao ni pamoja na vibali vya kuingiza na kutoa mbolea nchini na kusajili Mbolea.

Aidha amewakaribisha watembelee banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) lililopo katika maonesho ya biashara ya 46 ili kupata elimu ya mbolea, matumizi sahihi ya mbolea lakini kwa upande wa Wafanyabiashara amewakaribisha kupata ujuzi jinsi ya kupata leseni kupitia mfumo wa Mtandao.

Amesema mtandao huo unapatikana kwenye mtandao wa tovuti ya Mamlaka hiyo wa https: www.tfra.go.tz
Kaimu MenejaTehama na Takwimu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Salehe Kejo akizungmza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika 
Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakizungumza na Mfanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) leo Juni 30, 2022 wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya kibiashara ya 46 yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad