HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2022

MABEYO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UWANJA WA GOFU, HOTELI YA NYOTA TANO, KITUO CHA MICHEZO IHUMWA DODOMA

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akipata maelezo mradi wa ujenzi kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hotel ya nyota tano na kituo cha michezo Meja Amanzi Mandengula wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akikata utepe kuashiria  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi huo eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Dodoma
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akiweka jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akiendelea kukagua mradi wa  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akicheza mchezo wa Gofu kuashiria uzinduzi wa Mradi wa  wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara,akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la kujenga taifa JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akitoa taarifa ya mradi wa Ujenzi wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.

Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Wananchi wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo (hayupo pichani),akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka  jiwe la Msingi  ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu Dodoma
MKUU wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo ameweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hotel ya nyota tano na kituo cha michezo vinavyojengwa katika eneo la Jeshi Ihumwa Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Jenerali Mabeyo,amesema kuanza kwa ujenzi katika eneo hilo ni hatua nzuri katika kuimarisha mchezo wa Gofu nchini na kufungua fursa nyingi za kimichezo.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa uwanja huo ni wa kwanza kujenga jijini Dodoma lakini ni wa pili wa mchezo wa Gofu kujengwa na Jeshi hilo hapa nchini,ambapo wa kwanza ni ule wa Gofu uliopo Lugalo mkoani Dar es Salaam.

“Huu ni mwanzo mzuri katika kuimarisha mchezo huo hapa nchini ambapo mchezo huo umeanza kuwa maarufu sana na tumeanza na uwanja huu lakini lengo letu ni kujenga viwanja kama hivi nchini nzima ili kusisimua hamasa ya mchezo huo” Amesema Jenerali Mabeyo.

Amesema kuwa lengo la kujenga viwanja vya michezo ni pamoja na kuisapoti serikali katika kuendeleza michezo hapa nchini,ili watanzania wazidi kuipenda michezo pamoja na kupanua wigo wa kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Naomba niipongeze kamati ya Ujenzi wa uwanja huu iliochini ya Mwenyekiti Brigedia Hassan Mabena imefanya kazi nzuri ya ubunifu wa uwanja huo,”amesema Jeerali Mabeyo.

Amesema michezo ina umuhimu mkubwa kwa rika zote kiafya hivyo kukamilika kwa uwanja huo utasaidia watu kukusanyika katika eneo hilo na kupata burudani huku jeshi likiingiza kipato na kusaidia kuinua uchumi wa jeshi.

Hata hivyo amewatakaMajenerali na Maofisa wa Jeshi hilo kujifunza kucheza mchezo wa Gofu na michezo mingine ili wapatapo muda wa kushiriki mashindano ya nje wajitokeze kwa wingi kama wanavyofanya wanamichezo wengine.

“Kuna mashindano ya ngazi mbalimbali Jeshini,hivyo wakijifunza michezo itasaidia kutoa ushindano pindi mashindano yanapotokea,”almesema Jenerali Mabeyo.

“Nimefurahishwa na kituo hiki kitakuwa pia na academy kwa mchezo wa Gofu hii naimani itasaidia sana kukuza mchezo huo hapa nchini na itakuwa nchi ya tatu kwa kuwa na academy” Amesema.

Akizungumzia ujenzi wa kituo cha michezo mingine katika eneo hilo ambalo litakuwa na viwanja vya michezo mbalimbali pamoja na ujenzi wa hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano.

Jenerali Mabeyo amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo utasaidia kuongeza uchumi katika jiji la Dodoma kwani itatoa ajira za moja kwa moja na za muda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la kujenga taifa JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema eneo hilo lina ukubwa wa ekari 523 ambapo maandalizi yameanza ambapo mbali na ujenzi wa uwanja wa Gofu vitajengwa viwanja vya vingine mbalimbali ikiwamo Hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano.

Brigedia Jenerali Mabena,amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha michezo utagharimu zaidi ya bilioni 59 na kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho utainua hadhi ya makao makuu ya nchini na kupitia kituo hicho kitawaongezea mapato kupitia fedha za viingilio na ada.

Aidha ametaja baadhi ya viwanja vitakavyojengwa katika kituo hicho ni Uwanja mkubwa wa Gofu, uwanja wa mpira wa Miguu wenye uwezo wa kuchukua watazamaji elfu kumi(10,000), uwanja wa Tenis, Mpira wa Kikapu, Bwawa kubwa la kuogelea lenye hadhi ya Olimpiki na kituo cha michezo ya watoto.

Nae Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara,amesema kuwa yalikuwa ni matamanio yake ya muda mrefu ya kuwa na uwanja mkubwa wa gofu Dodoma na kila kanda ili kuinua ari ya mchezo huo nchini.

“Namshukuru Jenerali Venance Mabeyo alituahidi kuwa lazima ataanza uwanja wa Gofu na ametimiza ahadi yake na sasa uwanja huo unaanza kujengwa ambao utakuwa ni hazina kubwa katika kukuza mchezo huo h nchini” Amesema Jenerali Waitara.

Aidha amewaasa watanzania kutoogopa mchezo huo kwani hauna gharama kubwa kama watu wanavyoongea na kubainisha kuwa katika kituo hicho cha michezo itakuwa kama chuo cha mchezo wa Gofu nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Gofu Union (TGU) Chris Martin ,amelishukuru Jeshi hilo kwa kusapoti michezo hapa nchini,hususani mchezo wa Gofu kwa kuendelea kujenga viwanja vya mchezo huo na michezo migine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad