HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 25, 2022

KONGAMANO LA VIJANA LA SHINA INC LAFANA MAKUNDUCHI ZANZIBARKongamano la Vijana lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limefanyika katoka Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.

Akifungua Kongomano hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Suluhu amesema kuna watu wanahoji ni kwanini Shirika hili litoke Tanzania Bara na lije kufanya kazi Zanzibar tena Makunduchi mtu kama huyu kiukweli hajui masuala ya Muungano kwa mtu anayeelewa masuala ya Muungano kiujumla wake tunanzungumzia Tanzania na Tanzania inapatikana kwa Tanzania Bara na Zanzibar

Pia amesema katika kongamono hili amefuurahishwa na mada tatu zilizokuwa zinawasilishwa ni mada zinazohusu Vijana na mustakabali wa maisha yetu kwa ujumla hasa kwenye kwenye Uongozi na Utawala  inabidi kuzungumzwa kwa ufasaha zaidi ili watu wafahamu nini Uongozi na nini Utawala.

Amesema vijana wanashindwa kufahamu masuala hayo na ndio wanasababisha vijana wengi kuwatukana viongozi wao lakini kama wangepewa elimu mwanzo wasingeweza kwenda tofauti na maadili ya nchi.

Amewaomba watoa mada kuweza kwenda kwa kina ili vijana waweze kufahamu masuala yote ambayo watayatoa yote hapa.

Naye Rais wa Shirika la SHINA INC, Jessica Mushala amesema shirika hilo linajiendesha lenyewe kwa pesa zao ikiwa ni kurudisha kwa jamii hasa nyumbani Tanzania kwani wanaulizwa mara nyingi kuhusu wapi wanatoa pesa za kusaidia jamii lakini wao wamewiwa kusaidia jamii ili kuweza kuwainua watu walioko chini na ambao hawana uwezo.

Amesema Shirika la SHINA INC aliamini kwenye kutoa pesa kwa mtu mmoja mmoja kwasababu mtu anachokiona au anachojifunza   hakuna mtu anaweza kujua kilicopo kichwani mwake kwasababu hiyo ni zawadi kubwa zaidi.

“Tujifunze kuwa na moyo wa kutoa maana kutoa sio utajiri na kama watu wangeweza kutoa lakini ukimwambia mtu kutoa hata elfu 10 hawezi kutoa na anaweza kukutajia sababu nyingi” alisema Mushara.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Suluhu akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limefanyika katoka Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.
Rais wa Shirika la SHINA INC, Jessica Mushala akizungumza  na wageni rasmi pamoja na washiriki wa Kongamano lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limefanyika katoka Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.
Mkurugenzi wa Shirika la SHINA Tanzania, Joanes Chamushara akitoa salamu pamoja na kumkaribisha Rais wa Shirika la SHINA INC, Jessica Mushala kwa ajili ya kutoa hotuba yake wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limefanyika katoka Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.
Bw. Abeid Mtwana Haji akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Suluhu wakati wa Kongamano lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limefanyika katoka Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Suluhu kwenye kongamano lililofanyika katika Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.

Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Unguja Rashid Suluhu( wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Shirika la SHINA INC, Jessica Mushala (wa Tatu kulia) pamoja na vingozi mbalimbali wakati wa kongamano lililofanyika katika Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad