HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 14, 2022

JESHI LA POLISI WAKABIDHIWA PIKIPIKI NA KAMPUNI YA HERO, WAASWA KUTUMIA KWA LENGO LILILOKUSUDIWA

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya temeke. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Karimjee Jivanjee LTD, Willium Kadiva na kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumane Muliro Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akikata utepe kushiria kuzindua Pikipiki leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki hizo kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke.

Mkuu wa Wilaya ya Tekeme, Jokate Mwegelo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Richard Ngole wakiwa wamepanda pikipiki mara baada ya kukabidhiwa leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam zikiwa ni pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke.
Watumiaji wa pikipiki wakiwa wamepanda leo Juni 14,2022 mara baada ya kukabidhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Richard Ngole akikabidhi funguo kwa watumiaji wa Pikipiki leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumane Muliro akimkabidhi Nyaraka za pikipiki Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Richard Ngole leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumane Muliro akimkabidhi funguo ya pikipiki Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Richard Ngole leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama wilaya ya Temeke.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalunu ya Dar es Salaam, Muliro Jumane Muliro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Richard Ngole akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke.
Mkurugenzi Mkuu wa Karimjee Jivanjee LTD, Willium Kadiva akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya pikipiki tano kwaajili ya kusaidia ulinzi na Usalama katika wilaya ya Temeke. 


Maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa katika makabidhiano ya Pikipiki Tano aina ya Hero Hunter leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam.

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema kuwa jambo la Kampuni ya Toyota kupitia kampuni tanzu ya Hero kutoa pikipiki aina ya HERO HUNTER kwa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke tangu Jeshi la Polisi kuanzishwa kwake hapa nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wakati wa Makabidhiano ya pikipiki tano za Hero Hanter 125 cc kwa Jeshi la Polisi kwaajili ya kusaidia katika Ulinzi na Usalama katika Wilaya ya Temeke, makabidhiano hayo yamefanyika leo Juni 14, 2022 jijini Dar es Salaam amesema kuwa viongozi wa serikali wanahakikisha maeneo yanabaki salama.

Amesema makabidhiano ya PikiPiki hizo zinaenda kuwasaidia kupambana na Uhalifu ndani ya wilaya ya Temeke.

"Tunaendeleza kazi kwa kuhakikisha maeneo yetu yanabaki salama watu hawawezi kuendelea
kuendelea kufanya kazi kama maeneo hayako salama na sisi jukumu letu.... Sio kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, uongozi ni sehemu ya kutafuta suluhu hata kama sehemu ni ngumu kiasi gani...

Makabidhiano haya ya leo ya pikipiki yatasaidia jeshi la polisi kupambana na uharifu.." Amesema Jokate

Amesema mapambano dhidi ya wahalifu ni jukumu letu sote na jamii kwa ujumla, jukumu la kutoa taarifa za waharifu hata kama ni dada zetu, mama zetu hata kama ni mtoto wetu kwasababu wengi wamegundua wahalifu wanatokana na jamii, wanalindwa na jamii, wanalindwa na jamii na wanafadhiliwa ile jamii kwa maana akitoka huko akirudi pale watu wananunua TV kwa bei ambayo ni chini.

Joketi ameishukuru Familia ya Karimjee Jivanjee kwa kutoa msaada wa Pikipiki tano pia amesema kuwa kufanya biashara kwenye eneo ambalo lina usalama na biashara zinabaki salama na kufanyabiashara kwenye eneo ambalo halina usalama biashara nazo zinaathirika.

"Ni lazima tushirikiane katika suala la usalama sekta binafsi ishirikiane na serikali, jamii ishirikiane na serikali tukishirikiana pamoja matatizo yanabaki historia." Amesema Jokate

Hata hivyo amewaalika wadau wengine kushirikiana na wilaya ya Temeke katika kutatua changamoto mbalimbali iwe ya kiusalama, iwe ya kiulinzi ama ya kijamii.

"Kwa wale ambao wataendelea kuguswa tukipata hata pikipiki 50 ni jambo la heri... Katika kutusaidia kupambana na uharifu." Amesema Jokate

Hata hivyo amewaomba jeshi la Polisi pikipiki hizo wazitunze na zifanye kazi ambazo zimekusudiwa katika wilaya ya Temeke ili wananchi waendelee kuishi kwa usalama na amani.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amewashukuru Kampuni ya Hero kwa Kutoa Pikipiki aina ya Hero Hunter 125 cc zitakazo saidia kutokomeza uharifu katika Wilaya ya Temeke.

"Mmetutia Moyo, mmetupa nguvu, mmetupa silaha, mmetupa zana za kiutendaji za kupenya vichochoroni.... Tutapenya barabara zitashangaa na waharifu watashangaa!!.. amesema Muliro

Amesema kwa kuthamini zana hizo amewatadhalisha askari wenzake... Pikipiki hizi zisitumike vibaya, zisiwe kero kwa wananchi wema, zisitumike kufanya barabara zikashangaa kwa watu kuchukua kufanya vitendo vya rushwa au kumsaidia mhalifu na kusindikiza mhalifu au kumlinda mhalifu, piki piki hizi zitumike kuleta suluhu ya usalama kwa wananchi lakini ziwe mwiba mkali kwa waharifu..... Amesema Muliro.

Ametoa wito kwa makamanda wa wilaya nyingine za jiji la Dar es Salaam kuiga mfano wa kamati ya usalama ya Temeke.

Akizungumzia juu Ufanyaji kazi wa Pikipiki aina ya HERO HUNTER, Mkurugenzi Mkuu wa Karimjee Jivanjee LTD, Willium Kadiva amesema kuwa Hunter 125CC ni mchanganyiko mzuri wa mtindo na nguvu kwa sababu ya uchumi wake wa chini wa mafuta wa 50Km kwa lita, ni pikipiki bora zaidi kwa doria ya siku hadi siku na kudhibiti uhalifu.

Pia amesema kuwa inakuja na USB ya kucharge inayowaruhusu maafisa kuweza kuwasiliana kila wakati na bila kupoteza mawasiliano, ina pia matanki bora ya ujazo wa lita 13, inanafasi yakutosha na kiti chake kinauwezo wa kubeba mtu ofisa mwingine pia ina eneo lakubebea hati tofauti za maofisa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad