HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 2, 2022

DKT. STERGOMENA AONGOZA UFUNGUZI WA MAONESHO YA ZANA, TEKNOLOJIA YA KIJESHI

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Maenesho Madogo ya Zana na Teknolojia ya Kijeshi ya India (India Mini Defence Expo) jijini Dar es Salaam, Maonesho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) katika picha ya pamoja na washiriki wa Maonesho ameongoza Madogo ya Zana na Teknolojia ya Kijeshi ya India (India Mini Defence)

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameongoza Ufunguzi wa Maenesho Madogo ya Zana na Teknolojia ya Kijeshi ya India (India Mini Defence Expo). Maonesho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania. Maonesho hayo yamefanyika tarehe 30 Mei, 2022 katika Hoteli ya Hyatt Regency (iliyokuwa Kilimanjaro Hoteli), jijini Dar es Salaam.

Katika Maenesho hayo, makampuni mbalimbali yaliwasilisha mada mbalimbali kuhusu zana na vifaa vya kijeshi vinavyozalishwa na makampuni hayo nchini India. Katika Maonesho hayo ambayo Mheshimiwa Waziri akiwa Mgeni Rasmi alipata fursa ya kutembelea zana na vifaa hivyo na kupatiwa maelezo kuhusu zana na teknolojia hizo.

Kufanyika kwa Meonesho hapa nchini kunafuatia ombi la Balozi wa India kwa Serikali kupitia kwa Mheshimiwa Waziri Maonesho ya kibiashara kufanyika hapa nchini kuwawezesha wadau wa masula ya Ulinzi waweza kujionea zana mbalimbali zinazozalishwa India. Pamoja na kuwapa fursa wazalishaji na wasambazaji wa zana na vifaa kuja Tanzania kwa lengo la kuonesha bidhaa zao.

Akiongea na washiriki wa maonesho hayo, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesema “Tanzania na India zimekuwa na ushirikiano wa kindungu na wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali hususan kupitia sekta ya ulinzi, lakini pia, Maonesho hayo ni moja ya mambo yatakayoendelea kudumisha ushirikiano huo’’.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amebainisha kuwa “ushirikiano baina ya Tanzania na India umedumu tangu enzi za utawala wa Waasisi wa mataifa haya mawili, ambao ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Jamhuri ya India, Hayati Pandit Jawaharlal Nehru na kufuatiwa na hayati Mahatma Gandhi”.

Tangu kuaanzishwa kwa ushirikiano huu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la India (India Armed Forces) kwa pamoja yameendelea kuimarisha ushirikiano huu, kupitia maeneo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya kijeshi, huduma za tiba, mazoezi ya pamoja baina ya majeshi ya wanamaji, mapambano dhidi ya ugaidi na maeneo mengine mengi.

Maonesho hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa India nchini Tanzania, Balozi Binaya Srikanta Pradhan, ujumbe wa Ngazi za juu kutoka Serikali ya India, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule, wafanyabiashara kutoka India, Maafisa wa Kijeshi kutoka Tanzania na Jeshi la India pamoja na wadau wengine wa masuala ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad