HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 27, 2022

BRELA YAWAPIGA MSASA MAAFISA BIASHARA MTWARA, LINDI, PWANI NA DAR ES SALAAM

 

Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa akizungumza katika semina ya siku tatu iliyowakutanisha Maafisa Biashara kutoka katika Mikoa minne ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Mtwara na Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Biashara hao

Na Khadija Kalili
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Usalini wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amewataka maafisa biashara kutoka nje ya Ofisi zao ili kwenda kuzitambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzipatia utatuzi.

Akizungumza leo katika semina ya siku tatu iliyowakutanisha Maafisa Biashara kutoka katika Mikoa minne ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Mtwara na Pwani.

Katika semina hiyo Maafisa Biashara hao pia wametakiwa kutumia fursa za kukutana na wafanyabiashara katika Mikoa yako pamoja na kuangalia namna watakavyoweza kubuni fursa mpya za biashara ili kuweza kukuza kipato na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amewaeleza Maafisa Biashara hao kuwa kuwa anawaagiza wakajifunze kusoma bila kuchoka na kuhakikisha wanazingatia mafunzo hayo na pindi watakaporudi katika Mikoa yao waweze kuonyesha matokeo chanya ya mafunzo waliyoyapata.

"Hivi Sasa mafunzo kama haya ni muhimu kwenu ili kufanya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassani katika kuvutia wawekezaji katika nyanja ya biashara nchini hii hatima iko mikononi mweni kwani jukumu la kukuza uchumi wa nchi kunaanzia ngazi ya Mkoa." Amesema Kunenge.

"Fursa hii ni nzuri hivyo ni matarajio makubwa ya serikali kwenu Maafisa Biashara ingieni mtaani mkasikilize kero za wafanyabiashara" Amesema Kunenge.

RC Kunenge ameongeza kwa kusema kuwa lazima Maafisa Biashara wayajue huduma bora ambazo wanapaswa kuzitoa kwa wananchi na zipi hawapwi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad