HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

Benki ya NMB yasaidia ukusanyaji wa Trilioni 8.6 za Serikali

 


Benki ya NMB kupitia mifumo yake mbali mbali ya malipo imesaidia Serikali kukusanya trilioni 8.6 kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna wakati wa warsha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla, Wakuu wa Wilaya, madiwani, watendaji na waweka hazina

Zaipuna alisema benki yake imeendelea kuwekeza kwenye teknolojia jambo ambalo limesaidia kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi huku akisisitiza kuwa benki yake imejizatiti kuendelea kutoa bidhaa zinazokidhi mahitaj ya wateja wake.

“Ubunifu ni kitu pekee ambacho kimetusaidia kupiga hatua na ule uwekezaji ambao tuliufanya kwenye teknolojia ulituwezesha kuwa benki ya kwanza kuunga mifumo yetu na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na hadi sasa zaidi ya taasisi 1,100 tayari zimeunga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato,” alisema.

Zaipuna alisema ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kielektroniki umekuwa ukongezeka kutoka 2.1 trilion mwaka 2019 hadi 3.7 trilioni mwaka jana.

“Fedha hizi zilikusanywa kupitia mifumo yetu ya NMB mkononi, NMB Wakala, Lipa Namba, intaneti nk. Tunaendelea kuwekeza kuhakikisha kuwa mtandao wetu upo vizuri na kuhakikisha usalama wa malipo,” Alisema.

Aidha, Zaipuna alisema benki yake imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya jamii nchini kote nakuongeza kuwa benki yake kwa makusudi ilizindua taasisi yake ya NMB Foundation ilikuchangia maendeleo endelevu.

Alisema Benki yake kwa makusudi iliamua kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kuchangia maendeleo nchini kote kwenye sekta za elimu, afya, kilimo, mazingira, uwezeshaji na matukio ya dharura.

Zaipuna alisema benki yake itaendelea kushirikana na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo serikali ilikuleta maendeleo chanya na endelevu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla wakati wa warsha hiyo alishukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono jitihada mbali mbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Makala alisema utendaji mzuri wa benki hiyo umetokana na mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yamewekwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akisisitiza kuwa Serikali itandedelea kuboresha mazingira ya kubiashara ilikuvujia wawekezaji wengi nchini.

“Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli zetu za serikali. Serikali ina hisa kwenye benki hii na juzi tu wametoa gawio kwa serikali. Tutaendelea kushirikiana na Benki ya NMB ili kuboresha mazingira ya wananchi wetu,” alisema Makalla.

Makalla aliitaka benki hiyo kuendelea kubuni bidhaa mbali mbali zinazogusa wananchi kuanzia ngazi ya chini na kusisitiza kuwa Serikali itaendela kuchangia ushirikishwaji wa kifedha.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad