Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii, Dk. Francis Michael amewataka wadau wa utalii mkoani Arusha
kutumia fursa ya mikopo nafuu ya Benki ya NMB katika kuwekeza kwenye
sekta ya utalii ili kuvutia wageni nchini.
Akizungumza katika
kongamano la utalii (Tourism Networking) lililofanyika jijini Arusha
mwishoni mwa wiki Dk. Michael alisema Benki ya NMB imekuwa chachu katika
kuhakikisha inawapa mikopo wadau wa sekta ya utalii katika kuimarisha
mazingira ya vivutio nchini.
"Tunaomba mfanye jitihada za
kuijenga sekta ya utalii kwani serikali imeshaweka mazingira ya
kuitangaza kupitia filamu ya Royal Tour ambapo hadi sasa kuna baadhi ya
hoteli zimeshajaa wageni, hivyo ni kitu cha kujivunia kwetu na nyie kama
wadau ni vyema mkatumia fursa hiyo katika kuweka mazingira sawa,"
alisema Dk. Michael.
Dk. Michael aliwaeleza wadau wa utalii
kutumia vema fursa waliyopewa na Benki ya NMB kwa sababu ni taasisi
muhimu ya kifedha inayoshiriki kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi
na ubunifu nchini.
Alisema, fedha watakazotengewa kwa ajili ya
mikopo wazitumie vema ili wazirudishe na wengine wapate fursa ya
kuzipata kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza idadi ya watalii nchini
kwa maendeleo ya sekta zote.
Alisisitiza kuwa, wadau wa utalii
wahakikishe wanatumia vema fursa waliyopewa na NMB kikamilifu ili
kuimarisha usalama kwa watalii wanapokua nchini, ikiwemo kutumia vituo
vya polisi vinavyohudumia watalii lengo likiwa ni kuongeza idadi ya
watalii na kuwafanya wapate sababu za kurejea tena baada ya kurudi kwao.
“Hiki
kinachofanywa na NMB ni kitu kikubwa sana, kifikirieni na mkitumie
vizuri kwa sababu fursa kama hizi haziji mara mbili. Wafurahisheni
watalii ili wakienda kwao wakawalete watu wengine na wao warejee tena na
tena,” alisema Dk. Michael.
Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja
Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema benki hiyo wanaendelea kuunga
mkono juhudi za Serikali kuboresha sekta ya utalii nchini. Aidha, Mponzi
alisisitiza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni NMB imeanza kutoa huduma ya
mikopo katika sekta ya utalii lengo ni kuimarisha katika kutoa huduma
kwa wageni wanaofika nchini kutalii na kuona vivutio vilivyopo nchi
nzima.
"Bado tunaendelea kutoa katika sekta ya utalii kwa lengo
la kufanya vizuri zaidi na sasa tumejipanga kuwahudumia wageni wote
wanaofika nchini, ili wakirudi kwao wapate sababu ya kurejea tena
nchini," alisema Mponzi.
Benki ya NMB wiki kadhaa zilizopota
walikutana na wadau wa utalii visiwani Zanzibar ambapo waliwaahidi
kuwapa mikopo mbalimbali kuanzia maboti na miradi mingine
itakayohamasisha watalii kutembelea visiwa hivyi vyenye utajiri wa
historia na mambo ya kiasili.Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Francis Michael akisalimiana na
wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi
na Biashara, Filbert Mponzi (Kulia) wakati wa kongamano la wadau wa
Utalii lililofanyika jijini Arusha.
Afisa
Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi
akizungumza na wadau wa Utalii wakati wa Kongamano lililofanyika jijini
Arusha. Benki ya NMB iliwakutanisha Wadau wa utalii zaida 150
ilikujadili mbinu za kuboresha biashara zao.
Wednesday, May 25, 2022

Home
HABARI
WIZARA MALIASILI NA UTALII YAWATAKA WADAU WA UTALII KUTUMIA FURSA YA MIKOPO NAFUU YA BENKI YA NMB KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UTALII
WIZARA MALIASILI NA UTALII YAWATAKA WADAU WA UTALII KUTUMIA FURSA YA MIKOPO NAFUU YA BENKI YA NMB KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UTALII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment