HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 15, 2022

WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA BAGAMOYO SUGAR

 Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited ili kukagua utekelezaji wa mradi huo.


Tumekuja kukagua maendeleo ya mradi huu kujua kama unachangamoto zozote tuweze kuzitatua alisema Dkt. Kijaji.

Mradi huo ambao unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kwa sasa umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake.

Waziri kijaji amesema mradi huu ni moja ya Ushuhuda kuwa mpango Mkakati wa Taifa wa kuhakikisha Agenda ya Tanzania ya Viwanda vya kimkakati ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa muhimu hapa nchini unafanikiwa kwa kushirikiana na Sekta binafsi.

Tunatarajia kurudi hapa tarehe tano mwezi wa saba kwani tumeahidiwa mradi utakuwa umeanza uzalishaji kama walivyotuahidi.

Ajira za moja kwa moja Kampuni hii itakapokuwa imekamilisha uwekezaji wake tunatarajia kuwepo kwa jumla ya ajira za moja kwa moja zaidi ya 1500 za na zisizokuwa za moja kwa moja ni 3000.

Thamani ya Mradi Na Manufaa Ya Mradi kwa Watanzania
Kampuni hii inatarajia kuwekeza jumla ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 193.75 ambazo zitawekezwa katika kilimo cha miwa, miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa kiwanda, ununuzi wa mitambo, na vifaa mbalimbali vinavyohitajika..

Mahitaji ya Sukari na uzalishaji
Mahitaji ni kati ya tani 550,000-600,000 kwa mwaka na inatarajiwa kupanda hadi kufikia tani 800,000. Kiasi kinachozalishwa kwa sasa ni takribani tani 300,000.

Mradi huu unatarajiwa kuzalisha tani 30000 utakapoanza na utakapokamilika phase zote tatu utazalisha tani laki moja (100,000) za sukari kwa mwaka.

Serikali inafanya maboresho mbalimbali ili kuboresha mifumo na kurahisisha utoaji wa huduma zote za vibali na usajiri kwa wawekezaji.

Lengo ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto zote za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa haraka ili wawekezaji waweze kuwekeza miradi yao waliokusudia katika kipindi husika bila kukwamishwa na huduma za Taasisi.
 zetu.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akipoa taarifa ya mradi wa kiwanda cha kusindika sukari na shamba la miwa la Bagamoyo Sugar Limited, mali ya Makampuni ya Bakhresa, kutoka kwa Mratbu wa Mradi wa huo,Hussein Sufia (katikati)
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiangali sehemu ya kuchukulia maji yanayo kwenda shamba la miwa la Bagamoyo Sugar linalomilikiwa na makampuni ya Bakhresa wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari na shamba la miwa la kampuni hiyo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)




Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akikagua shamba la miwa la Bagamoyo Sugar linalomilikiwa na makampuni ya Bakhresa wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari na shamba la miwa la kampuni hiyo wilayani Bagamoyo wa kushotoMratbu wa Mradi wa Makampuni ya Bakhresa , Hussein Sufia.(Pich na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)







Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za ujezi wa kiwanda hicho
ziara ikiendelea
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha kusindika sukari na shamba la miwa la Bagamoyo Sugar Limited, mali ya Makampuni ya Bakhresa, leo Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na viongonzi mablimbali.Watumishi wa TIC wakiwa katika Picha ya Pamoja.
(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad