HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 15, 2022

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA BALOZI WA KOREA YA KUSINI NCHINI KUHUSU UJENZI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU


SERIKALI imeuelekeza uongozi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inajenga meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu kuzingatia makubaliano yote yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa meli hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Mei 14, 2022 katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.

Katika Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania Bw. Kwak ambaye alikiri mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo na aliahidi kuwa kampuni yake itaongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa wakati na meli hiyo iwezo kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa.

Pia, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza kuwa watalaamu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania warejeshewe Pasi zao za kusafiria ambazo zilizuiwa na Serikali kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mwenendo wa ujenzi wa meli hiyo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Mbarouk Mbarouk na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Mwakibete.

Wengine ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli, Philemon Bagambilana na Kanali Samwel Mahirane ambaye ni Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini.

 



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kati yake na Balozi wa Korea Kusini Nchini, Kim Sun Pyo (kulia) kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Kanali Samweli Mahirane, Kamishina wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini na Balozi Caesar Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo baada ya mazungumzo kati yao kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2022. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Kanali Samweli Mahirane, Kamishina wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini na Balozi Caesar Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo kati yao kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2022. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk (kulia kwa Waziri Mkuu) , Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete (kulia) , Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dong Myung Kwak (aliyesimama nyuma katikati), Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (nyuma kushoto) , Kanali Samweli Mahirane, Kamishina wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini (nyuma kulia) na Balozi Caesar Waitara ambale ni Mkurugenzi wa idara ya Asia na Australia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki (kushoto). Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad