Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe
amezindua Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji jijini Dodoma na kuwataka
wajumbe wa bodi hiyo kutumia taaluma zao na uzoefu walionao kazini
kuisimamia na kuishauri Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mhe, Bashe ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutengeneza Kanzidata
inayoonyesha yalipo maeneo yote yanayofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji
nchini ambayo ni Hekta Milioni 29, kuandaa upembuzi yakinifu na usanifu
wa kina kwa maeneo yote yafaayo kwa kilimo cha Umwagiliaji ikiwemo
ukanda wa Mto Rufiji, ukanda wa ziwa Victoria kuanzia Mwanza hadi
Kagera, Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa,Mto Ruvuma na bonde la Kilombero
pamoja na taarifa ya mazao yanayostawi katika maeneo hayo ambapo pia
amesisitiza kuwa maeneo hayo yahifadhiwe kisheria kuwa maeneo ya kilimo
cha Umwagiliaji kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Mhe, BASHE
amesema Wizara yake itazitumia nafasi 800 zilizotolewa na Serikali
kuajiri wahandisi 143 wa Umwagiliaji watakao huduma katika Ofisi za
Wilaya zitakazofunguliwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Mwaka wa
fedha 2022 - 2023 ambao majukumu yao pamoja na mambo mengine ni
kusimamia Skimu za Umwagiliaji.
“Tunafungua Ofisi kila Wilaya
ili tuweze kusimamia kikamilifu Skimu tunazojenga,tumekuwa tukijenga
Skimu za Umwagiliaji alafu tunaacha zinasimamiwa na Chama cha Ushirika
tukitaraji kinasimamia vizuri, wanalima wao, wanavuna wao Banio
likiharibika wanakuja Wizarani kuomba fedha za kujenga Banio”
Aidha
Mhe, Bashe ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuweka Wasimamizi
katika Skimu zote 1,097,000 nchi nzima ambazo Serikali imewekeza kwa
kujenga Miundombinu kwa lengo la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa ada
na tozo za Umwagiliaji kwa mujibu wa Sheria.
“Kwa mujibu wa
takwimu, tunapoteza zaidi ya shilingi Bilioni miamoja kila Mwaka kwa
kushindwa kukusanya ada na tozo fedha ambazo zingesaidia kutunisha mfuko
wa Umwagiliaji na kuwezesha Tume kukopa Mabilioni ya fedha kwaajili ya
kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya Umwagiliaji”(megar project)
Akizungumza
kwa niaba ya Bodi, Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
Prof. Henry Mahoo amewataka Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi kwa kujituma ili kufikia malengo
yaliyowekwa na serikali.
“Tutatumia mbinu zozote kuhakikisha haya malengo yanafikiwa”
Kwaupande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond
Mndolwa ameahidi kuisimamia Taasisi anayoiongoza kwa weledi kufikia
matarajio ya wananchi hususani katika Kilimo cha Umwagiliaji.
Picha
ya pamoja kati ya Waziri wa Kilimo, Wajumbe wa bodi ya Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.Waziri
wa Kilimo Hussein Bashe wa saba kutoka kushoto.
Kulia kwa Mhe.
Waziri Bashe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof.
Henry Mahoo, na kushoto kwa Waziri Mhe, Bashe ni Mkurugenzi Mkuu wa
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa.
Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe akifafanua jambo kwenye kikao hicho
Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao cha pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe jijini Dodoma.
Monday, May 16, 2022

Home
HABARI
WAZIRI BASHE AZINDUA BODI TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI,AIPA MALENGO YA KIMKAKATI SEKTA YA UMWAGILIAJI.
WAZIRI BASHE AZINDUA BODI TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI,AIPA MALENGO YA KIMKAKATI SEKTA YA UMWAGILIAJI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment