HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 26, 2022

WAJOMBA, BABA, KAKA WATAKIWA KUWA MSAADA KWA WATOTO WAKIKE KUPATA HEDHI SALAMA

 Na Khadija Seif, Michuzi TV

KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya Hedhi salama ambapo uadhimishwa Kila ifikapo Mei 28 walezi na wazazi wakiume watakiwa kufuta fikra na dhana potofu katika kumsaidia mtoto wakike awapo katika Mzunguko wa hedhi Kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wahabari Mwanaharakati wa kusaidia jamii hususani swala la Afya, Asnat Masoud maarufu kama "Naswiat Brembo" wakati alipotembelea shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi iliyopo Magomeni fundikila jijini Dar es salaam, amesema watoto wakike wanapitia changamoto kubwa yakukosa kupata elimu ya namna wataweza kujistiri endapo linatokea swala la kupata Hedhi Kwa mara ya kwanza majumbani na hata Mashuleni.

"Wazazi wakiume wamekua watu wakujibagua na kuona ni kitu cha kuvunja Mila zilizojengeka kuwa hedhi ni aibu hivyo hawawezi kumpa msaada wiwote ule mtoto wakike badala yake mtoto anaachwa apate fedheha mbele za watu wanaomzunguka."

Hata hivyo Brembo amewahusia wanafunzi wa shule hiyo kuepuka ugonjwa wa shingo ya saratani ya kizazi Kwa kutumia vizuri taulo hizo na kuepuka kukaa nazo kimatumizi kwa muda mrefu zaidi au kutumia kifaa tiba ambacho sio salama kwao.

Sanjari na hilo Brembo amegawa boksi sita  za taulo zakike Kwa wafunzi hao ka sehemu ya kuadhimisha siku ya Hedhi salama ambapo kilele chake ni mei 28 mwaka huu.
Mwanaharakati wa kusaidia jamii hususani swala la Afya ya uzazi pamoja mjasiriamali wa vipodozi Asnat Masoud a.k.a Brembo akikabidhi taulo za kike Kwa Dada Mkuu wa Shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi iliyopo Magomeni findikila jijini Dar es salaam kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Hedhi salama ambapo uadhimishwa Kila ifikapo mei 28.

 picha ya pamoja kati ya Mjasiriamali wa vifaa tiba na vipodozi Asnat Masoud na wanafunzi wa shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi iliyopo Magomeni mara baada ya kuwagawia taulo zakike kama sehemu ya kuadhimisha kilele cha siku ya hedhi salama

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad