HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2022

WAJASIRIAMALI DAR WANUFAIKA NA ELIMU YA MTANDAO NA BIASHARA

 TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Karibu Culture Contact (KCC) ikishirikiana na taasisis ya Dira Women Association (DIWO) wamatoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake Wajasiriamali ili waweze kufanya biashara kwa kutumia Mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam leo Mei 18, 2022, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Karibu Culture Contact (KCC), Bhwai Nicodemus amesema kuwa Kipindi cha Corona (COVID-19) wanawake walikuwa wahanga wa kufunga biashara zao, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kufanya biashara katika hali zote.

Amesema kuwa katika mafunzo hayo watawafundisha namna ya kufungua Kurasa katika Mitandao ya kijamii ili waweze kuwafikia wateja wengi zaidi na kwa wakati mmoja.

Upande wake Mkurugenzi Wa Dira Women Association (DIWO), Shamsa Danga amesema mafunzo hayo yatawawezesha wajasiriamali hao kupata fursa za kufanyabiashara zao ndani ya nchi na kimataifa Zaidi.

“Leo watapewa maunzo kuhusu kufungua mtandao wa kijamii wa kibiashara, watapata elimu kuhusu kuanya iashara yenye tija kupitia mitandao, uzoefu wa ujasiriamali kitaia na kimataifa, jinsi ya kupata mitaji na uzoefu wa biashara za vikundi….” Amesema Shamsa

Akizungumza kuhusiana na wajasiriamali kufanya biashara  kitaifa na Kimataifa, Shamsa amesema tayari kunawajasiriamali walishiriki maonesho la Africa International festival lililoanyika nchi Ujerumani mwaka 2018 kwahiyo kupitia mafunzo hayo wajasiriamali wa nafasi kubwa ya kuomba kushiriki maonesho hayo.

“Kupitia semina hii ya leo tunawahamasisha washiriki wa mafunzo haya leo waweze kuanya maombi yakwenda kufanyabisahara za kimataifa Zaidi.” Amesema Shamsa

Amesema waliowahi kushiriki maonesho ya kibiashara nchini Ujerumani pamoja na Wachoraji, wachongaji vinyago, wasonaji wa nguo na wajasiriamali wa kazi za ubunifu.

Mwakilishi wa wajasiriamali waliohudhuria mafunzo hayo, Mkurugenzi wa taasisi ya mama Mzalendo Tanzania Art, Leila Abdala amesema mafunzo hayo yatawasaidia katika kupanua wigo katika biashara yake, kuwaelekeza watoto yatima kutumia mtandao katika kujipatia kipato.

Kwa Upande wa Mjasiriamali Joyce Fadhil amesema kuwa mafunzo hayo yatamwezesha kutumia mitanao ya kijamii ili kuwafikia watu wengi Zaidi katika kutangaza biashara yake hapa nchini na nje ya nchi.
Baadhi ya washiriki wakizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2022, wakati wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wanawake wajasiriamali kufanya biashara zao kwa kutumia mtandao.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Karibu Culture Contact (KCC), Bhwai Nicodemus akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2022, wakati wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wanawake wajasiriamali kufanya biashara zao kwa kutumia mtandao.
Mkurugenzi Wa Dira Women Association (DIWO), Shamsa Danga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2022, wakati wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wanawake wajasiriamali kufanya biashara zao kwa kutumia mtandao.
Mkufunzi kutoka  Dira Women Association (DIWO), Farida Nassoro akizungumza na Wanawake wajasiriamali jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2022, wakati wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wanawake wajasiriamali kufanya biashara zao kwa kutumia mtandao na namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali. 


Mjasiriamali Joyce Fadhil akizungumza na waandishi wa habari namna mafunzo ya biashara na mtandao yatakavyowasaidia.
Mkurugenzi wa taasisi ya mama Mzalendo Tanzania Art, Leila Abdala akizungumza na waandishi wa habari namna mafunzo ya biashara na mtandao yatakavyowasaidia.

Baadhi ya washiriki wa Maunzo ya biashara ya mtandao yanayotolewa na KCC wakishirikiana na DIWO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad