HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 16, 2022

UTEKELEZAJI ANWAN ZA MAKAZI WAFIKIA ASILIMIA 90,ZOEZI KUWA ENDELEVU- KASPAR MMUYA

 



Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
NAIBU Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspar Mmuya ameeleza, Zoezi la anwani za makazi limefikia asilimia zaidi ya 90 ,licha ya baadhi ya maeneo kumalizia marekebisho machache hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Pwani, kwa niaba ya Waziri Mkuu ,ambapo amefika kujionea utekelezaji wa mkoa , kuangalia uhalisia ikiwa Ni kipindi kifupi kimebakia kufikia 30 Mei 2022 ,kufanya marekebisho machache wanayoyabaini kwenye mfumo na ziara mbalimbali.

Mmuya alieleza, licha utekelezaji wa zoezi hilo kwa Sasa, litakuwa ni endelevu kutokana na mzunguko wa kimaisha ,( ongezeko la watu na makazi) ili Serikali iweze kuendelea kujenga mfumo mzuri wa mipango ya maendeleo na kiuchumi .

"Halmashauri nyingi ziliangalia nyumba kadhaa, tunahitaji viwanja navyo vipatiwe namba, inatakiwa muda tuliopewa na Rais tufanye maboresho, kujua uhalisia na viwanja vilivyopo,vinavyojengwa ,na visivyojengwa ,Sisi Tuna deal na viwanja navyo viwe na namba'"

"Kila mmiliki awe na namba na ni wajibu wake mtu akijenga awe na namba huo ndio msimamo wa Serikali"alisisitiza Mmuya.

Mmuya alisema, kutokana na umuhimu wa Zoezi hili litakuwa sio kwa ajili ya sensa pekee badala yake litakuwa endelevu ili kuirahisishia Serikali kupanga mipango kwa watu wake kulingana na ongezeko la watu na makazi kwa kila wakati.

Awali Ramadhani Mbura kaimu mkuu wa kitengo Cha TEHAMA Mkoa wa Pwani, alisema katika utekelezaji wa Jambo Hilo ,Hadi kufikia Mei 12 mwaka huu anwani za makazi 519,440 zimekusanywa na kuingizwa kwenye mfumo sawa na asilimia 106.43.

Akaongeza kueleza kuwa,miundombinu ya barabara 17,407, vimepewa majina,Majengo ya viwanja 919,440 zimeainishwa .

"Vibao 2,087 vya namba za nyumba zimetengenezwa na kubandikwa, nguzo 7,582 zenye mbawa za majina ya barabara za mitaa na Vijiji zimetengenezwa na kubandikwa., alifafanua Mbura.

Vilevile kwa mujibu wa taarifa kutoka TANROADS Pwani, imesema wamefanyia kazi maagizo ya Rais kwa asilimia 90, Ambapo hadi sasa Jumla ya vibao 88 tayari vimewekwa huku 83 kati yake vikiwa vimekamilika na vitano bado vinafanyiwa marekebisho.

Zoezi la kutambua anwan za makazi linaendelea nchini kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa kutambua na kuweka jina la mtaa wako, namba ya nyumba na postikodi ya kata ,licha ya kwamba tarehe ya agizo la Rais kikomo Ni Mei mwaka huu ,Lakini kutokana na umuhimu wake wa mipango ya kimkakati wa kimaendeleo italazimika Kuwa endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad