HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 23, 2022

Tunzaa yawakaribisha wafanyabishara kuuza bidhaa zao

 

Mkurugenzi wa Kampuni Tunzaa, Ng'winula Kingamkono akizungumza na waandishi habari kuhusiana na biashara ya kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali zikionyesha namna wanavyopata wateja kwa njia ya Mtandao

*Ni kwa njia mtandao wateja kulipa kidogo kidogo 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV 
KAMPUNI ya Tunzaa ya kununua bidhaa kupitia program Nununu (APP) imesema kuwa tangu kuanza kwake imeanza kuwa na wateja  wengi kwenye mtandao ambapo bidhaa zilizopo sokoni ni chache ambapo amewataka wafanyabiashara  kuingia makubalino na kampuni hiyo ili kuweza kuuza bidhaa zao.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Kampuni Ngw'inula Kingamkono amesema kuwa wanaonunua bidhaa kwa njia ya mtandao wamekuwa wengi ambapo bidhaa zingine wanazikosa ambayo ni fursa ya wafanyabiasha kuingia na Tunzaa na kufanya biashara kutokana na uhakika wa soko.

Amesema kuwa ununuzi wa bidhaa katika maduka mbalimbali ni kuweka kidogo kidogo katika mfumo wa malipo ndani ya Tunzaa na mara kukamilika malipo ndipo mteja atapata bidhaa mahali popote alipo kama alivyotoa pendekezo lake.

Kingamkono amesema hadi sasa wateja hadi sasa wamefikia 12000 ambapo mwitikio mkubwa ambao haundani na bidhaa hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kujiunga ili kwenda kuwafikia wateja kwa wingi.

Amesema mfanyabiashara anayetakiwa ni wale walio katika mifumo ya biashara wanamaduka yaliyosajiliwa ili kuendelea kuweka imani kwa wateja.

Aidha amesema lengo ya kampuni ni kuona wafanyabishara wanafikia matarajio yao kwani kufanya biashara na kampuni ya Tunzaa kutawafanya bidhaa zao kutoka kwa haraka na kuagiza bidhaa zingine na kufanya kumudu ulipaji wa kodi pamoja na huduma zingine katika biashara.

"Tunzaa ipo katika kufanya biashara zikuwe kwani wateja wa kulipa kidogo kidogo ni wengi kuliko wa kulipa kwa pamoja lakini hivyo suluhu imepatikana kuanzisha Tunzaa ambapo wafanyabiashara ndio watatoa huduma ya mahitaji ya jamii" amesema Kingamkono

Hata hivyo amesema wateja wengi wamekuwa wakiuliza vifaa vya ujenzi na magari ambapo hakuna wafanyabiashara walioko katika mfumo wa Tunzaa.

Amesema licha ya kuanzisha hiyo wamekuwa wakitoa huduma nyingine ya kutengeneza teknolojia ikiwa ni pamoja ya kuwainua vijana waliosomea masuala ya tekonolojia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad