HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2022

TCRA kutoa Masafa na namba maalum bure kwa watafiti


Wanafunzi wakiwa katika banda la TCRA katika Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

 Na Mwandishi Wetu Dodoma

MAMLAKA  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatoa masafa pamoja namba maalum za kutoa huduma bure kwa watafiti wote watanzania wanaofanya tafiti zinazolenga katika kutumia Teknolojia ya mawasiliano kuongeza tija katika shughuli mbalimbali nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Ubunifu nchini yanayofanyika mkoani Dodoma Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa TCRA Mabel Masasi amesema utaratibu huo unalenga katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha ufanyaji wa tafiti ambazo zinalenga katika kuleta maendeleo nchini.

Akizungmzia jinsi ya kupata masafa na namba kwa ajili ya utafiti Mabel amesema iwapo watafiti wanafanya utafiti kupitia vyuo basi vyuo vyao vinatakiwa kuwasiliana na Mamlaka hiyo ili kuweza kukamilisha taratibu za kupata masafa au namba ya kufanyia utafiti bila kulipia.

Kuhusu watafiti binafsi wanaotaka kufanya utafiti kwa kutumia rasilimali hizo Mabel amesema watafiti binafsi watatakiwa kwenda kujisajili Costech ambapo kupitia wao wataweza kuombewa rasilimali hizo kwa ajili ya utafiti bila kulipia.

Madhimisho ya ubunifu hufanyika kila mwaka ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni Ubunifu kwa maendeleo endelevu.

Afisa Mkuu  Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma
Afisa  Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Aika Benson akimpa maelezo ya shughuli za mamlaka kwa mteja aliyetembelea maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya Ubunifu yanayofanyika jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad