HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2022

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA ITC KUWEZESHA WAZALISHAJI WA ASALI KUFIKIA SOKO LA KIMATAIFA

 Afisa Program Kituo cha Biashara cha Kimataia (ITC) Aman Goel akizungumza wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.Na Karama Kenyunko Michuzi TV

MAMLAKA ya Biashara nchini TanTrade kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) wametoa fursa kwa wauzaji wa asili nchini na kuwapatia mafunzo ili kulifikia soko la Kimataifa.

Aidha wazalishaji hao wa asali wametakiwa masoko kuzalisha asali bora itakayokithi viwango vya kimataifa.

Imeeleza kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali Afrika ikiongozwa na Ethiopia na kwamba asali yake ni ya asilia na ina viwango vya ubora.

Akizungunza kwenye warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini leo Mei 10, 2022 Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Masha Hussein amesema kuwa Tanzania ipo kwenye mpango maalamu waliokubaliana na nchi za umoja wa ulaya kwa ajili ya kuwawezesha wafugaji nyuki kuendana na matakwa ya soko la kimataifa.

Amesema kuwa asali ya Tanzania inaubora kutokana na kuwa na misitu mingi na kwamba ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na Asali bora.

Alisema kuwa tayari wamefungua soko la asali nchini Saudi Arabia na kampuni zaidi ya 10 zimeanza kufanya biashara ya kuuza asali na kwamba wanaendelea kuhamasisha wafanyabiashara wengine ili kwenda kufanya biashara.

"Asali yetu ni asilia kwani ina kitu cha ziada ambacho hakipo kwenye asali nyingine kwa sababu ya misitu. Changamoto zilizopo katika asali yetu katika kupata masoko ni ufungashaji wa bidhaa baada ya uzalishaji hivyo, tunasisitiza katika ufungashaji ili kupata masoko zaidi," amesema Hussein.

Amesema kigezo hicho kitaifanya Tanzania kuwa kinara kwenye soko la kimataifa ambapo kwa sasa Tantrade kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Biasha (ITC) litawewezesha wafugaji wa kitanzania kutoa asili yenye viwango na ubora wa kimataifa.

"Tanzania ni ya pili kwa Afrika kwa kuwa na asali bora shida ni kwamba hatujakuwa na ufungashaji bora hivyo Tantrde tutaendelea kushirikiana na wadau wengine kuwezesha wafugaji na wafanyabiasha wetu kuhakikisha kuwa wanakidhi vigezo vya soko la kimataifa"

Amesema kuwa Tantrade imewapatia wafanyabiasha kutoka kwenye kampuni kumi soko la Asali la nchi ya Kifalme ya Saud Arabia.

Kwa upande wake, Mratibu Taifa wa programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki (Bevac) inayofadhiliwa na umoja wa ulaya Magdelena Muya amesema kuwa mradi huo utakwenda kuwanyanyua kiuchumi wafugaji wa nyuki kwa kuingia kwenye mnyororo wenye thamani kwa kuuza Asali.

Amesema kuwa mradi huo unaotiwa nguvu na wizara ya Maliasili utawawezesha wafugaji kupata vifaa vya kisasa vya ufugaji sambamba na kupewa maeneo maalum yatakayokuwa hifadhi ya ufugaji nyuki pamoja na kulindwa kwa sheria maalum.

"Wafugaji nyuki wanapata changamoto sehemu za ufugaji mara nyingi vifaa vyao vinaibiwa kwa hiyo tutafungua maeneo ya hifadhi ya ufugaji nyuki na yatalindwa kwa mujibu wa sharia" amesema Magdelena.

Amesema kuwa kwenye mradi huo wafugaji , wachuuzi na wafanyabiashara wa kimataifa wa asali watapewa mafunzo.

Naye, Ayoub Kamwaga mfugaji nyuki ushirika wa Kibondo Kigoma wanaotumia mizinga ya kisisa amesema kuwa changamoto kubwa ya shughuli hizo ni soko ambapo akipatikana mnunuzi mmoja analimiki soko na kujipangia bei ya kununua jambo ambalo haliwanufaishi.

Amesema kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwao kwa kuwa itapanua soko la kuuza asali zao.

Amesema kuwa mradi huo umewezesha kupata ujuzi wa kutengeneza mizinga ya kisasa na kuvuna asali yenye ubora zaidi.
Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Masha Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mfugaji nyuki ushirika wa Kibondo Kigoma, Ayoub Kamwaga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mratibu Taifa wa programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki (Bevac), Magdelena Muya akizungumza wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mshuri wa Taifa kutoka taasisi ya ITC na kitongo cha Eco System, Dino Woiso akizungumza wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Kituo cha Biashara cha Kimataia (ITC), Aina Dalo akifafanua jambo wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wadau wa wafugaji nyuki, wachuuzi wa asali pamoja na wafanyabiashara wa Asali wa kimataifa nchini wakiwa katika warsha iliyofanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad