Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
akizungumza katika kikao chake na watumishi wa sekta ya ardhi mkoani
Mbeya.
Sehemu
ya watumishi wa sekta ya ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (Hayupo pichani) wakati
wa kikao chake na watumishi wa sekta hiyo mkoani Mbeya.
Kamishna
wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mbeya Siyabumi Mwaipopo akizungumza wakati wa
kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani
Kikwete na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Mbeya.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Zakariyya Kerra (Kulia) akiandika maelezo wakati wa kikao kati ya
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
na watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Mbeya.
Mkuu
wa wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuwachuwa akizungumza katika kikao kati
ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
na watumishi wa Sekta ya Ardhi mkoa wa Mbeya
Na Munir Shemweta na Anthony Ishengoma, WANMM MBEYA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete
amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuhakikisha wanatoa haki
wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.
Alisema,
utoaji haki uko katika sura tofauti kuanzia zoezi la utoaji hati,
upatikanaji haki katika mabaraza ya ardhi na nyumba sambamba na utoaji
taarifa na uwezeshaji wananchi katika ardhi au rasilimali ardhi.
Alisema,
baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi wamekuwa miungu watu kwenye
maeneo yao kuliko hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye
ardhi yote iko chini ya mamlaka yake na kubainisha kuwa, mwananchi
anaweza kwenda ofisi ya ardhi kwa ajili ya kumilikishwa ardhi lakini
adha anayoipata wakati wa kuomba kupata uhalali wa kumiliki ardhi yake
basi maafisa ardhi wamekuwa wakijizungusha bila kumsaidia.
‘’kama
nilivyokwisha sema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, uabaishaji
ufike mwisho tumeelewana ndugu zangu’’ alisema Rdhiwani.
Naibu
Waziri Kikwete alieleza hayo tarehe 13 Mei 2022 alipokutana na
watumishi wa Sekta ya Ardhi Mkoa wa Mbeya ambapo alioneshwa
kutoridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya watumishi wasiowaadilifu.
‘’Kama
kuna mtumishi anadhani kuna suala la kula kula ovyo kwenye Wizara hii
ya ardhi basi siyo kwa nyakati hizi, ndugu zangu watendaji wenzangu
naomba tuwe waadilifu katika kutenda haki kwa wananchi.’’ Alionya
Ridhiwani Kikwete Naibu Waziri Wizara ya Ardhi.
Sambamba
na hilo aliwataka Maafisa Mipango miji wa Mkoa wa Mbeya kuwa na mipango
bora ya mipango miji ili jiji Mbeya lisiendelea kuwa jiji la makazi
holela.
Kwa
mujibu wa Ridhiwani, ukiwa kwenye ndege unaona milima ya mbeya
imejengwa majengo kwenye ardhi isiyopimwa ambapo aliwataka Maafisa
Mipango Miji hao kutosubiri watu kuendeleza makazi holela na baadae
kujitokeza kurasimisha maeneo hayo.
‘’Acheni
kusubiri wananchi wajenge alafu nyie muwafuate kuendeleza mipango miji
badala yake muwe wa kwanza kupima na kupanga miji ili wanachi waishi
kwenye makazi bora tofauti na sasa mnapowaa na kusababisha kuaribu
milima na taswira ya jiji la Mbeya’’ alisema Ridhiwani.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete yuko
mkoani Mbeya kwa ziara ya siku mbili ambako mbali na na kufanya kikao na
watumishi wa sekta ya ardhi ameshiriki zoezi la utoaji hati na leseni
za makazi kwa wananchi wa halmashauri ya jiji la Mbeya pamoja na wale wa
Mamlaka ya Mji mdogo wa Mbalizi.
No comments:
Post a Comment