KAMISHNA
Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee mapema leo amezindua
miradi ya Gereza Kuu Uyui,Tabora. Miradi hiyo ni mradi wa Duka, Mashine
ya kusaga, majengo ya biashara. CGP Mzee amepongeza juhudi hizo za
kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mema anayoyafanya kwa
Jeshi na Taifa kwa ujumla.
KAMISHNA
Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee mapema leo akikagua
samani mbalimbali zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Samani Uyui,
Tabora. CGP Mzee amehimiza Kiwanda hicho kuzingatia maboresho hususani
ubora na bei yenye uhalisia.
Baadhi ya Samani mbalimbali zinazotengenezwa na katika Kiwanda cha Samani Uyui, Tabora. Kiwanda hicho kipo Gereza Kuu Uyui.
Baadhi
ya Maofisa na askari wa Gereza Kuu Uyui wakiwa timamu kwa ziara ya Mkuu
wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee(hayupo pichani).
KAMISHNA
Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akiwasili Gereza
Nzega kwa ziara ya kikazi mkoani Tabora. CGP Mzee amepongeza mabadiliko
na juhudi za maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi katika Gereza la
Nzega.
Ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Gereza Nzega, Tabora ukiendelea katika hatua za awali(msingi) kama inavyoonekana pichani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akikagua nyumba za askari Gereza Uyui, Tabora.
Muonekano wa nyumba za maafisa na askari wa Gereza Kuu Uyui, Tabora.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee(katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na askari wa Gereza Kuu
Uyui, Tabora mara baada ya kutembelea Gereza hilo leo Mei 16, 2022.
Picha zote na Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment