HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 16, 2022

MDEE NA WENZAKE KUENDELEA NA UBUNGE WAO

 MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesema wabunge 19 wa Chadema (Covid 19) waliovuliwa uanachama wa chama hicho hivi karibuni wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania mpaka pale Mahakama itakaposikilza maombi yao ya zuio la muda Juni 13, 2022.


Uamuzi huo umetolewa na Jaji John Mgeta leo Mei 16, 2022 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Mapema, Mdee Mdee wenzake 18, kupitia wakili wao Aliko Mwamanenge Mwamanenge waliwasilisha mahakama hapo maombi namba 13 ya mwaka 2022 ambayo ni maombi madogo kwenye shauri la msingi namba 16 la mwaka 2022 wakiomba mahakama kurejeshewa uanachama wao .

Uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa wabunge hao umefanywa wiki iliyopita na baraza Kuu la chama hicho.

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya bodi ya wadhamini ya Chadema, Tume ya Taifa ya uchaguz na AG.

Katika maombi hayo Mdee na wenzake wamefungua maombi ya zuio la muda wakiomba waendelee kuwa wabunge hadi uamuzi wa maombi yao ya leave yatakapotolewa.

Baada ya kuwasilishwa kwa maombi hayo, mjibu maombi namba moja na mbili, Wakili wa serikali Mkuu Gabriel Malata ameiomba mahakama kuwapatia muda wa ili wa waweze kupitia maombi hayo na kuwasilisha kiapo kinzani.

Akijibu hoja za mleta Maombi, Wakili Peter Kibatala na Jeremiah Mtobyesya ambao ni wajibu maombi wa kwanza, wanaoiwakilisha Chadema wamewasilisha hoja sita za kupinga kukubaliwa kwa zuio hilo mahakamani hapo ambazo zilizojikita kwenye madai ya kasoro zilizopo kwenye hati ya kiapo cha waombaji.

Kibatala amedai Mahakamani hapo kiapo kina dosari ya kutotanabaishwa dini za waapaji (Mdee na wenzake), "Viapo vyao mahitaji dini zao ikitokea wanataka kuupa wataapa kwa kitabu gani?".

Hoja nyingine Kibatala amedai Mahakamani hapo waombaji wameomba waendelee na Nyazifa zao bila kueleza hoja hiyo zinakwenda kwa nani kama ameelekezwa Spika wa Bunge au Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

"Oda za Mahakama hunyooka zinatekelezeka".

Kibatala amesema kuwa waombaji wameomba nafuu ya kuendelea kuwa wanachama wa Chadema bila kubainisha nafuu hiyo waipate kwa nani.

Hoja ya Mwisho Kibatala ameiomba Mahakama hiyo kutumikia mbali zuio hilo kwa kiapo hiko hakijakidhi sharti la zuio la kuwa wanaomba zuio juu ya hatari gani.

Upande wa waombaji Mwamanenge, amesisitiza mahakama kutoa amri ya zuio hilo kwa upande wa wajibu maombi hakuwa na hoja za kutosha kuzuia mahakama kutotoa zuio hilo kwa kuwa hawajaweka wazi sheria ipi inataka unataka waapaji wateja dini zao.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote tatu, Jaji Mgeta amesema kuwa mahakama hiyo inazuia wabunge hao kuondolewa kwenye nyazifa zao mpaka tarehe 13 Juni ambapo mahakama itasikiliza mashauri yote mawili.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad