HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 24, 2022

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA JENGO LA UFUNDI TOWER KATIKA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Zelot Stephene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Saidi Issa ambaye ni Meneja wa Ktengo cha Uzalishaji, Chuo cha Ufundi Arusha kuhusu ujenzi wa Jengo la Ufundi Tower wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la jengo hilo jijini Arusha, Mei 24, 2022.
Waziri Mku Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa na Mwanachuo wa Chuo cha Ufundi Arusha, Michael Felix (kulia) wakati alipoweka jiwe la msing la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24,2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha wakipiga makaofi kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad