HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 23, 2022

Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship waiomba Serikali kufanya uchunguzi sehemu alipo 'Mzee wa Yesu'

 

Baadhi ya waumini na viongozi wa kanisa wakifatilia tamko la kanisa kuhusiana na kutoweka kwa Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.

Mama Mteule wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship,  Greener Mkombo  akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu kutojulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.
Kuhani wa Kristo wa Kanisa la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship Nazar Nicholaus  akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu kutojulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama 'Mzee wa Yesu'.
*Wadai Serikali ina Mkono mrefu wa kujua aliko Mzee wa Yesu

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KANISA la House of Prayers Shield of Faith Christian Fellowship limeiomba Serikali kusaidia kujulikana alipo Askofu wa Kanisa hilo Mulilege Kameka maarufu kama Mzee wa Yesu.

Ombi hilo limetolewa Mei 22, 2022 jijini Dar es Salaam na Kuhani wa Kristo Nazar Nicholaus akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni Siku saba zimepita tangu kutoweka kwake licha juhudi kufanyika.

“Rai kwa Serikali, tunachotaka kujua ni Askofu Mulilege yupo wapi ili aweze kuhudumiwa kwani hadi sasa tumeshazunguka kila mahali ikiwemo kwenye vituo vya Polisi lakini hatujamuona,” amesema Nicholas na kuongeza kwamba.

“Tumemua kuongea na vyombo vya habari Rais asikie pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwani Rais ameshaiweka nchi kwenye Sheria."

Nicholaus amesema kwamba tangu wamezungumza juu ya hilo Jumatano iliyopita bado hakuna jipya hadi leo juu ya taarifa za aliko Mzee wa Yesu.

“Tunaamini Serikali ina mkono mrefu hakuna kitu kinaweza kufanyika wahusika wasijulikane, amesema Nicholaus.

Hata hivyo Nicholaus amesema wataendelea kumtafuta na kufanya maombi bila kuchoka ili kuhakikisha Askofu anapatikana.

Kwa upande wake Mama Mteule wa Kanisa hilo ambaye pia ni Mke wa Mzee wa Yesu Greener Mkombo amefichua kwamba tangu mwaka 2011 amekuwa akisumbuliwa kwa madai kwamba sio Raia wa Tanzania.

Kwamba tatizo hilo lilianza mara tu walipohamia jijini Dar es Salaam wakitokea mkoani Mbeya.

Hata hivyo amesema pamoja na hayo Mzee wa Yesu amekwisha shinda kesi na Mahakama Kuu kuthibitisha kwamba ni Mtanzania.

Hivyo amesisitiza Serikali kusaidia kupatikana kwa Mzee wa Yesu ili kama anashikiliwa kwa makosa yoyote aweze kufikishwa Mahakamani ili mkondo wa Sheria uchukuliwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad