HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 25, 2022

ELIMU YA SENSA, KATA KWA KATA LUDEWA

 

Na. Damian Kunambi, Njombe

Ikiwa tunaelekea mwezi wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu kote nchini Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imeunda timu zitakazo ongozwa na viongozi wakuu wa wilaya hiyo ambazo zitapita na kutoa elimu katika kata zote 26 za Wilaya ya Ludewa ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa kikamilifu.

 Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Sensa wilayani humo mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema sanjari na kupita katika kata hizo lakini pia watatumia viongozi wa dini mbalimbali ili waweze kuelimisha waumini wao katika nyumba za ibada.
"Viongozi wa dini na madhehebu yote tutawaomba watangaze wao wenyewe suala la Sensa tena ikiwezekana wanukuu baadhi ya vifungu vilivyopo katika vitabu vya dini, ambavyo vinaelezea zoezi la kuhesabu watu".

Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratius amesema ili kuweza kufanikisha zoezi hilo wanapaswa kujitoa hivyo tayari ofisi yake imefanya maandalizi ya magari kwaajili ya kusafirisha timu hizo.
"Tunapaswa kujitoa na kujigawa kwa makundi ili kazi yetu iweze kwenda vizuri, mimi nitatoka na kundi langu, mkuu wa wilaya atatoka na kundi lake vivyo hivyo kwa mwenyekiti wa Halmashauri na tutasambaa maeneo tofauti tofauti ya wilaya hii".

Aidha kwa upande wa mmoja wa wanakamati wa kikao hicho Thomas Kiowi ambae ni Afisa maendeleo ya jamii alitoa mapendekezo ya kufikisha elimu hiyo mapema kwa baadhi ya kata za tarafa ya mwambao ambako asilimia kubwa ya wakazi wake ni wavuvi na wanakawaida ya kusafiri maeneo mbalimbali kwaajili ya shighuli hizo za uvuvi huku Alex Henjewele ambaye ni mratibu wa Sensa wilayani humo amesema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku 10.

Pamoja na mikakati hiyo ya kufanikisha zoezi hilo la sensa, lakini bado kumeonekana kuwepo kwa baadhi ya changamoto ya kimiundombinu katika maeneo ya tarafa za mwambao na kwingineko ambapo watalazimika kupita kwenye mapori kwa kutembea kwa miguu kutokana na kutokuwa na barabara huku wakazi wake wakiushi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad