HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 27, 2022

DC NAMTUMBO APONGEZWA KWA KUSIMAMIA VYEMA UTEKELEZAJI WA ILANI

 

 NA  YEREMIAS NGERANGERA, NAMTUMBO

Hayo yamesemwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Ramadhani abbas suleiman (Mcheju) wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kibanio kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji uitwao ‘’Mradi wa ukarabati Namtumbo mjini.”

Suleimman alidai chama katika wilaya ya Namtumbo kinajivunia kupata kiongozi ambaye anafuatilia utekelezaji wa ilani bega kwa bega kwa kushirikiana na viongozi wa chama na wananchi wa wilaya ya Namtumbo alisema katibu huyu.

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya hiyo Aggrey Mwansasu pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya huyo alisema kitendo cha mkuu wa wilaya huyo kujitosa kutembea kwa mguu zaidi ya kilomita 8 msituni ni kitendo cha kutaka kuwatumikia wananchi kwa vitendo na sio maneno.

Mwansasu alidai umbali wa kilomita nane katika maeneo ya milima mikali sio mchezo lakini mkuu wa wilaya huyo alitembea kwenda kuona eneo linalojengwa kibanio ili kujiridhisha upatikanaji wa maji mara baada ya mradi kukamilika kwa kujionea mwenyewe na sio kuambiwa.

Hata hivyo Mwansasu alisema viongozi wa chama na serikali kwa pamoja watashirikiana kwa pamoja kueleza kwa wananchi kuhusu juhudi za serikali katika kutatua kero za upatikanaji wa maji Namtumbo mjini kwa kupitia mradi huo.

Mhandisi wa RUWASA wilaya ya Namtumbo David Mkondya alisema mradi wa ukarabati Namtumbo mjini unatekelezwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia fedha za wafadhili kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19.

Aidha Mkondya alidai gharama ya mradi wa kukarabati Namtumbo mjini ni shilingi 1,669,359,689.36.ambapo kiasi cha shilingi 409,982,860.36 ni gharama za kazi zitakazotekelezwa na mkandarasi huku kiasi cha shilingi 101,950,000. Tayari kimetumika kwa malipo ya awamu ya kwanza kwa mkandarasi na kiasi cha 1,259,376,829,kimetumika kwa ajili ya kununulia mabomba na RUWASA makao makuu kutoka kampuni ya PLASCO.

Mradi wa ukarabati Namtumbo mjini unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 20 juni 2022 na mkataba wake wa awali ulisainiwa tarehe 14 mwezi januari 2022 na ulitarajiwa kukamilika tarehe 20 mei 2022 ambapo ulishindikana kukamilika kutokana na changamoto ya daraja ya mto luegu iliyosombwa na maji na kusababisha ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi huo wakati wa kusafirisha vifaa na mkandarasi kuomba kuongezewa muda mpaka juni 20 mwaka huu.

Mhandisi Stanley Mlelwa wa kampuni ya SIVIKWA CO Ltd.alidai mwezi juni 2022 tarehe 20 atakamilisha mradi huo kwa kuwa mradi huo umefikia asilimia 60 katika utekelezaji wake

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu baada ya kufika katika eneo linalojengwa kibanio hicho alijionea uwezo wa mto kuwa na maji mengi ,kajionea uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo na kuwataka viongozi wa chama na serikali wilayani Namtumbo kuungana kwa pamoja ili kuendelea kuhimiza na kukataza wananchi kuharibu mazingira ya misitu ambayo ni chanzo cha mito.

Mradi huo wa ukarabati Namtumbo mjini ukikamilika  utawanufaisha wananchi 36,779 kutoka mitaa ya Namtumbo kati,Rwinga,Minazini,Libango na sehemu ya migelegele.

Kibanio(Intake) inajengwa katika mto Likiwigi katika kijiji cha Libango ambapo mkuu wa wilaya alipongezwa kwa kutembea kwa miguu kufika katika sehemu inapojengwa kibanio hicho umbali wa kilomita 8.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad