HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 11, 2022

Zaidi ya ekari 10 zasombwa na maji Ludewa, Mbunge alia na wananchi wake

Mashamba ya mahindi yalivyoathiriwa na mafuriko.

Na Amiri Kilagalila, Njombe
Zaidi ya ekari kumi za mashamba katika kijiji cha Kiyogo kata ya Masasi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zimesombwa na maji baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha April Mosi mwaka huu na kuwaacha wananchi wakihangaika namna ya kupata chakula.

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa wananchi hao wameeleza kwa jinsi gani mafuriko hayo yamewaletea athari huku wakiwa na hofu juu ya upatikanaji wa chakula.

“Wengine zimesombwa ekari tano maji yamezoa kila kitu hatuna Mahindi wala mihogo familia zinalia hakuna chakula na hapa tunaokoteza tu yaliyobaki na maji”

“Na baadhi ya wananchi karibu nyumba nane walikuwa hawana hata pa kukaa na kama maji yale yangebaki basi tungekuwa na maafa makubwa sanaa ila mifugo Ng’ombe mmoja alikufa na mbuzi wawili walikufa tunaomba serikali ituangalie wananchi wa Kiyogo”alisema mwananchi

Miongoni mwa Viongozi waliofika kujione hali ilivyotokea ili kutafuta namna ya kuwasaidia wananchi hao ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga na hapa anaeleza kwa jinsi gani alivyoguswa na tatizo hilo.

“Wakazi 667 wote mazo yao yamepata majanga hayatafaa tena kwa matumizi ya binadamu kwa hiyo tunawaza wananchi hawa wataishi vipi,na kwasababu tupo kwenye vikao vya Bunge nitalipeleka serikalini ili kuona hawa wananchi wanasaidiwaje”alisema Kamonga mbunge wa jimbo la Ludewa.

Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba ya wananchi wa Kiyogo yaliyopatwa na maafa.
Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga akitazama jinsi miogo ilivyoathiriwa na mvua.
Namna mahindi ya wakazi wa Kiyogo yalivyookotwa baada ya mashamba yao kusombwa na maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad