HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 26, 2022

Waziri Bashungwa :Serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa akikabidhi vifaa vya Tehama Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Abdul Maulid kuwakilisha  Maafisa wa Mikoa wakati uzinduzi  usambazaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Vituo vya Walimu (Teachers’ Resource Centres- TRCs) katika hafla iliyofanyika  Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, Jijini Dar-es-salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi)Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa kuzindua usambazaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Vituo vya Walimu (Teachers’ Resource Centres- TRCs) katika hafla iliyofanyika  Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, Jijini Dar-es-salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa akikata utepe kuashiria kuzindua usambazaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Vituo vya Walimu (Teachers’ Resource Centres- TRCs) katika hafla iliyofanyika  Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, Jijini Dar-es-salaam.


Picha za makundi mbalimba katika uzindizi wa vya Tehama kwa vituo vya walimu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo  akizngumza kuhusiana na umhimu wa vifaa vya Tehama vilikabidhiwa kwa maafisa elimu mkoa katika shule ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rugwa akizungumza kuhusiana na mikakati ya mkoa wa Dar es Salaam kujenga shule kubwa ya wanafunzi 40000 wakati hafla ya kikabidhi vifaa vya Tehama kwa Maafisa Elimu Mikoa ,jijini Dar es Salaam.

*Amesema vifaa vya Tehama vinakwenda kuakisi mahitaji ya sasa ya Teknolojia Tehama

Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amesema kuna mapinduzi makubwa yamefanyika awamu ya sita katika sekta elimu kujenga miundombinu ya madarasa pamoja vitendea kazi kwa walimu lengo ikiwa ni kuhakikisa wanafunzi wanapata elimu bora.

Ameyasema hayoleo tarehe 25 Aprili, 2022 wakati wa kuzindua usambazaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Vituo vya Walimu (Teachers’ Resource Centres- TRCs) 150 vilivyopo katika Halmashauri 144 za Mikoa 26 ya Tanzania Bara luliofanyika Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, Jijini Dar-es-salaam.

Waziri Bashungwa amesema vifaa hivyo vinakwenda kutatua changamoto kwani vituo vikiwepo bila vitendea kazi kuna kuwa hakuna umuhimu wake

Katika uzinduzi huo wa vifaa vya Tehama Waziri Bashungwa amewaagiza ,Makaatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha wanawasilisha taarifa ya mapokezi na usambazaji wa vifaa hivyo kimkoa kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais – TAMISEMI kabla au ifikapo tarehe 15 Mei, 2022;

Amewataka Makatibu hao kuhakikisha wanasimamia ufundishaji na ujifunzaji ili matokeo ya Mitihani ya Taifa na Ubora wa Elimu viendane na kiwango kikubwa cha uwekezaji unayofanywa na Serikali..

Amesema kuwa Serikali imeamua kuvifufua vituo hivyo kwa lengo kusaidia walimu kubadilishana uzoefu, hali kadhalika wataalam wabobezi kupeana mbinu za ufundishaji wakiwa na walimu, ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu ya msingi na sekondari nchini.

Ameendelea kufafanua kuwa hadi sasa tayari Halmashauri 144 zimeanza kutekeleza Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA). Walimu 12,544 tayari wameshapatiwa mafunzo, na lengo ni kuwafikia walimu 30,957 katika mwaka huu wa fedha.

Waziri Bashugwa ameziagiza Halmashauri zote nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023 kuhakikisha wanatenga bajeti ya maeneo ya kujenga vituo hivyo vya TEHAMA ili Halmashauri zote nchini zoweze kuwa na vituo hivyo muhimu katika kipindihiki chenye mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia

Aidha vifaa vilivyogawiwa ni mashine ya kudurufu 150, printa 150 projekta 150 na kompyuta za mezani (desktop computers) 600 vilivyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.5

Bashungwa aliwataka wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, kutenga fedha kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo ili lengo la serikali la kutoa elimu stahiki kufikiwa nchini.

Mbali na hilo, alisema serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa kutoa elimu ya sayansi kwa njia ya Televisheni nchini.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI sekta ya elimu, Gerald Mweli, alisema serikali imeamua kufufua vituo vya kujifunzia walimu kwa kutoa mashine hizo za kisasa za TEHAMA.

Aliwataka walimu wote wanaolengwa kufikiwa na huduma hiyo ili nao watoe elimu inayoendana na viwango vya kimataifa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa amesema Mkoa wa Dar es Salaam, unatarajia kujenga shule ya kisasa ya sekondari ya wanafunzi mchanganyiko, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita itakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 4,000.

Rugwa amesema Shule hiyo itakuwa ya bweni na inatarajia kujengwa katika mwaka mpya wa fedha wa 2022/23 na itakamilika mwisho mwa mwaka huu.

"Nikudokeze Waziri Bashungwa unaweza kuona shule hii ya Benjamin Mkapa ni kubwa sana kwa mkoa wetu kwa sababu unachukua wanafunzi zaidi ya 1,700, lakini tuna mpango wa kujenga shule bora ya kisasa ya mkoa itakayochukua wanafunzi wengi zaidi na ujenzi utaanza muda wowote kuanzia sasa,” alisema Rugwa.

Waziri Bashungwa alisema, vifaa vya TEHAMA vimetolewa kwenye vituo 150 vilivyopo nchini, kwa ajili ya walimu kujifunza na kufundishia somo la TEHAMA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad