HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 11, 2022

WANANCHI WAJITOKEZA KAMPENI YA SARATANI NJOMBE

 Na. WAF - NJOMBE

Wanaume tisa wakutwa na viashiria vya Saratani ya tezi dume ambao ni sawa na Asilimia 17 ya waliojitokeza kwenye kampeni ya uchunguzi wa saratani ya tezi dume mkoani Njombe.

Hayo yamebainishwa na Meneja Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Maguha Stephano kwenye kampeni ya uchunguzi wa Saratani iliofanyika mkoani Njombe na kuhudhuriwa na wananchi 600 huku wengi wao wakiwa ni akina mama.

Amesema Wanaume walijitokeza walikua 103 sawa na asilimia 17, waliopimwa na kukutwa na viashiria hivyo vya Saratani ya tezi dume na walipewa rufaa ya kwenda taasisi ya Saratani ocean road kwa uchunguzi zaid na matibabu.

Kwa upande wa Wanawake Dkt. Maguha amesema Wanawake waliojitokeza ni 497 sawa na asilimia 83 huku wanaume wakiwa 103 sawa na asilimia 17 na kufanyiwa vipimo vya magonjwa mbalimbali ya Saratani.

"Wanawake Saba ambao walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya matiti walikutwa na uvimbe na wawili walikuwa na viashiria vya Saratani ya matiti".

Pia, wanawake wengine waliofanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi 10 walikutwa na mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi (precancerous lesions) na walipatiwa tiba (cryotherapy) ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na wanawake wawili walikutwa na Saratani ya mlango wa kizazi na kupewa rufaa kwenda Ocean road.

Kampeni hiyo ya uchunguzi wa Saratani mkoani Njombe ilianza tarehe 8 mpaka 10 April, 2022 na kutolewa kwa wananchi wote bila malipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad