HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 17, 2022

WANAFUNZI KENYA NA TANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA MAHUSIANO

Na Humphrey Shao,Michuzi TV

Wito umetolewa Kwa Watanzania na Kenya kuongeza mahusiano ya kitaaluma bila kuangalia tofauti zao za Mipaka ya nchi zilizomo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa hivi Karibuni na Naibu Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ,Prof Patrick Nsimama wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 24 waliokuja kujifunza katika Chuo hicho kupitia mradi wa RAFIC.

Prof. Nsimama ametaja kuwa licha ya nchi zetu kutenganishwa na Mipaka lakini Bado ni Moja Kwa maana ya Jumuiya na Bara Zima la Afrika.

"DIT Ndio Sehemu pekee ambayo kinajengwa kituo Cha umahiri Kwa ajili ya ICT Kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki hivyo ni vyema Vijana na watumishi waliopo katika jumuiya kuja Tanzania kuchota maharifa yalipo katika kituo hicho" Amesema Prof.Nsimama.

Aidha Amesema licha ya kuwa tofauti ya Mipaka Bado wanafunzi wetu wameonyesha kuwa mitaala ya ufundishwaji ayatofautiani baina ya nchi na nchi  ndio maana wanafunzi Hawa 24 kutoka Kenya wamewwza kufanya vizuri katika mafunzo yao.

Ametaja kuwa wanafunzi hao wamewwza kujifunza Masuala ya Graphics Disigner ,Animation na Masuala ya Mtandao.

Naibu Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) ,Prof Patrick Nsimama wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi 24 waliokuja kujifunza katika Chuo hicho kupitia mradi wa RAFIC.
Mmoja wa Walimu kutoka Kenya walioongozana na wanafuzni kutoka Kenya akizungumza wakati wa hafla  kutunukiwa vyeti wanafunzi 24 kutoka kenya
Dr.Garden Tesha akizungumza na Wanafuzni kutoka Kenya 

Mratibu Radical na Mradi wa RAFIC ,Dr.Joseph Matiko akizungumz umuhimu wa mradi huo

Mmoja ya Wanafunzi kutoka Kenya akizungumza uzoefu wake katika Safari hii ya Mafunzo




 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad