Kupitia sera yake ya
uwajibikaji kwa jamii (CSR), Benki ya NMB imetenga asilimia moja ya
faida baada ya kodi kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali hususani
katika sekta za elimu, afya na majanga.
Katika ziara ya
watumishi wa Benki hiyo kwa mikoa wa Tabora, Kigoma na Shinyanga,
wameshuhudia wakazi wakinufaika na misaada hiyo na kueleza namna ambavyo
mchango wa NMB umekuwa chachu ya hatua kubwa za kimaendeleo kwao na
jamii kwa ujumla.
Kwa upande wa elimu, mashuhuda wameelezea
kuwa, tangu NMB iwape viti, meza na madawati kwa shule 23 mikoani humo,
ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka sababu wanakaa katika mazingira mazuri
wakiwa madarasani ambayo yamepelekea mahudhurio yao kuongezeka kwani
wanafurahia elimu.
Pamoja na hilo, NMB imeendelea kutoa vifaa
vya kuezeka katika shule (23)ambayo imepunguza wanafunzi kubanana katika
chumba kimoja na hivyo kusoma kwa nafasi bila bugudha.
Misaada
hii imewanufaisha walimu, “Tumekuwa wanufaikaji wakubwa na uwajibikaji
huu, kwani sasa kila mwalimu anafanya kazi yake kwa moyo mmoja na
kuhakikisha wanafunzi wanasoma na tunaufaulu mzuri” alisema Mwalimu
Mkuu, Joyce Munyu wa Shule ya Msingi Majengo.
Uwajibikaji wa
namna hii ni sehemu inayoifanya benki kuishi kauli mbiu ya ‘NMB Karibu
Yako’ lakini pia kuwa kinara na bora Tanzania.
Mwakilishi
wa wanafunzi wa shule ya sekondari Nkundutsi wilayani Kasulu , Kigoma
akizungumza kwa niaba ya wanafunzi walipotembelewa na maafisa wa Benki
ya NMB
Dada
mkuu wa shule ya sekondari Kisuke wilayani Ushetu akizungumza kwa niaba
ya wanafunzi wa shule hiyo walipotembelewa na maafisa kutoka Benki ya
NMB
Afisa
wa Benki ya NMB kutoka idara ya uwajibikaji kwa jamii, Aloyce Kikois
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Ushokola walipotemebelea
shule hiyo.
Tuesday, April 19, 2022

Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB yaendelea kugusa wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment