HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

TASISISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZAASWA KUJIENDESHA KIDIJITALI

Mkurugenzi Mkuu wa Media Convergence, Asha Abinallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa NGOYADIJITALI kwaajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali kujiendesha kidijitali uzinduzi huo umeanyika leo Aprili 28,2022 katika hoteli ya Srena jijini Dar  Es Salaam.
Mkurugenzi wa Tehama kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mulembwa Munaku akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa NGOYADIJITALI kwaajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali kujiendesha kidijitali uzinduzi huo umeanyika leo Aprili 28,2022 katika hoteli ya Srena jijini Dar  Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa C- Sema, Kiiya Joel akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa NGOYADIJITALI kwaajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali kujiendesha kidijitali uzinduzi huo umeanyika leo Aprili 28,2022 katika hoteli ya Srena jijini Dar  Es Salaam.
Baadhi ya wadau wa mashirika yasiyoyakiserikali wakiwa katika uzinduzi wa Mradi wa NGOYAKIDIJITALI leo Aprili 28,2022 Katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

TAASISI ya Media Convergence ikishirikiana na kampuni ya Meta wamezindua Mradi wa NGOYAKIDIJITALI kwaajili ya kuwasaidia mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini kujiendesha kidijitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Aprili 28,2022 Katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Media Convergence, Asha Abinallah amesema kuwa maradi huo utajikita katika maeneo manne ya Uendeshaji wa taasisi zisizo za kiserikali ili kujiendesha kidijitali.

Amesema kuwa moja ya Maeneo hayo ni pamoja na Uangalizi (Incubation), ambapo wataanza kufanya kazi na mashirika 35 ambayo yatakuwa yapo tayari kufanya kazi na taasisi hiyo kwa kuangalia mifumo ya kidijitali, kukagua mtiririko wa mawasiliano ya taarifa za kidijitali na kutoa ripoti pamoja na kuangalia na kutoa mafunzo kwa zana za meta na kulinganisha teknolojia.

Asha pia amesema kuwa watatoa mafunzo kwa watu 1000 ambapo mafunzo hayo yatafanyika kwa wiki mbili au tatu ili kila mlengwa wa mafunzo hayo apate kile ambacho kinafundishwa kwa ufasaha.

Licha ya hayo Asha amesema kuwa katika Mradi huo wataongea mara kwa mara na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali ili kila shirika liweze kujiendesha kidijitali.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Tehama kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mulembwa Munaku amesema kuwa Serikali inahakikisha kuwa Tanzania inakuwa ya kidijitali kwasababu mpaka sasa imeshajenga mkongo wa taifa wa mawasiliano ambao unaunganisha mawasiliano kutoka sehemu moja na nyingine.

Munaku amesema kuwa Mkongo huo umeshaunganisha mikoa yote ya Tanzania na pamoja na nchi saba zinazoizunguka, nchi hizo ni Kenya Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Mozambique na imebaki nchi moja ya Congo DRC ambapo kufikia 2023 itakuwa imeshaunganishwa na mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Amesema kuwa kwa upande wa mifumo serikali imeshawezesha utendaji kazi wa serikali pamoja na kuwezesha wananchi kutumia mifumo ya selikali.

Amesema kuwa Wizara imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba taasisi zinakuwa na mazingira wezeshi ya kuweza kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.

"Taasisi zote za serikali, sekta binafsi, Mashirika ya maendeleo wote watumie teknolojia ya habari na mawasiliano katika kufanya shughuli zao na katika utoaji huduma kwa wateja." Amesema Munaku

Munaku ametoa wito kwa taasisi zisizo za kiserikali ziweze kuangalia namna waweze kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano, pia amepongeza Taasisi ya Media Convergency kwa kuwaona taasisi zisizo za kiserikali kutumia teknolojia na kuwa kidijitali.

Kwa Upande wa Msajili wa taasisi zisizo za kiserikali, Vickness Mayao amesema kuwa mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yamekuwa hayatumii teknolojia ya habari na mawasiliano hivyo uzinduzi wa leo utawawezesha mashirika husika.

Amesema kuwa zaidi ya mashirika 12000 yalikuwa yamejisajili lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano kwa sasa kunataarifa hai za mashirika 7533 mpaka sasa kutokana na kutengeneza mfumo wa kujisajili.

Amesema kuwa umhimu wa Ukuwaji wa teknolojia ya habali na mawasiliano umesaidia kuwepo na data ambapo miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu kufuatilia kwa ukaribu.

"Nitoe wito kwa mashirika haya yasiyo ya kiserikali kutumia uzinduzi wa NGOYADIJITALI kama fursa na kutambua kwamba masuala ya kidijitali hayakwepeki." Amesema Vickness

Aidha ametoa wito kwa mashirika ya kiserikali kuwa na mifumo ya ukaguzi sa ndani na sio kuweka kila kitu kwenye vitabu na serikali inaangalia namna ya kuziwezesha taasisi hizo ili ziweze kuitumia ipasavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad