HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 25, 2022

Taasisi ya Doris Mollel, Amref Tanzania zawafikia Wananchi zaidi ya 400 mkoani Shinyanga

  
Katika kuadhimisha siku ya Malaria Duniani, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akiwa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini wakigawa vyandarua viliyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Amref Tanzania, kwa wanawake zaidi ya 400 na kufikia makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mollel ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Amref Tanzania kwa kuja na mkakati  wa kueliesha jamii juu ya janga la Malaria na kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuweza kutoa misaada mbalimbali inayogusa maisha ya Watanzania.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

"Asante wakina mama mliokuja hapa kupata elimu ili mkatusaidie kuelimisha wengine na kupunguza vifo vya akina mama na watoto" amepongeza Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel ambaye pia ni Balozi wa Watoto Njiti, Doris Mollel amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu ya ugonjwa wa malaria na namna ya kujikinga pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili waweze kujikinga na janga la korona, tunaliona linaisha ila bado ugonjwa upo.

"Zoezi limefanyika katika mikoa mitatu kwa kushirikiana na Amref, ambayo ni Simiyu, Kagera na Shinyanga na tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira wezeshi sisi taasisi binafsi kuweza kufanya kazi na kutoa mchango wetu ndani ya jamii" amesema Doris Mollel.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad