HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

Serikali kuweka mifumo rahisi ya kuendeleza wabunifu wa Tehema-Profesa Kipayula

 Mwakilishi wa Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu wa Wizara hiyo Profesa Maulito Kipayula  akimkabidhi cheti cha ubunifu mmoja wa Kikundi kilichobuni mashine ya Shurubati kupata mpaka uingizw fedha ya sarafu ya Shilingi 200 na 500 katika Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Dk.Jabiri Bakari akizingumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimaitafa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu wa Wizara hiyo Profesa Maulito Kipayula  akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Mkundwe Mwasaga akizungumza kuhusiana mwitikio wa Wasichana katika Tehama katika Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika Ukumbi wa Maktaba jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu wa Wizara hiyo Profesa Maulito Kipayula akipata maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Katoriki Iringa (RUCO )Jesca Katoke kuhusiana na ubunifu mashine ya Shurubati ya Kuongiza Sarafu kisha unapata shurubati   katika Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama iliyofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



Picha mbalmbali katika siku ya kimataifa ya Wasichana na Tehama iiliyofanyika Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

*Dk.Jabir asema ni asilimia 30 ya wasichana walioko katika Tehama
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SERIKALI imesema itahakikisha inaweka mifumo rahisi ya kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu kwa lengo la kuongeza idadi ya wasichana kwenye masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Aidha, amezitaka Mamlaka za mawasiliano kuhakikisha wanafikisha mawasiliano na kutatua changamoto ya mtandao vijijini ili wanafunzi wapate kunufaika na mapinduzi hayo ya Tehama.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Msichana katika Tehama na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Maulito Kipanyula kwa niaba ya Waziri, Profesa Adolf Mkenda.

Profesa Kipanyula alisema kuwa ni wakati wa kuhamasisha na kuwawezesha wasichana kuingia katika masuala ya Tehama ili angalau wafikie asilimia 50.

Alisema takwimu za Aprili 2022, zinaonesha kuwa Tume ya Sayansi imesajili wasichana 112 pekee sawa na asilimia 13 ukilinganisha na wanaume.

"Maendeleo ya sayansi na Teknolojia yapo mikononi mwa vijana hivyo, ni lazima mchangie katika kubuni vitu vyenye manufaa kwa Taifa. Pia kumuwezesha mtoto wa kike kuwa sehemu ya maendeleo ya Tehama," alisema Profesa Kipanyula.

Alisema kuwa wataendelea kusambaza vifaa vya Tehama katika shule zote za serikali ili kuongeza hamasa katika matumizi ya teknolojia na ubunifu.

Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Tehama, Dk Nkundwe Mwasaga alisema serikali itaendelea kuhakikisha usalama wa mtandao ili kukabiliana na utapeli, wizi wa utambulisho na unyanyasaji wa kijinsia.

Dk Mwasaga alisema sekta ya mawasiliano imekuwa kwani mpaka Desemba 2021 idadi ya watumiaji wa intaneti imeongezeka kufikia watu milioni 29 na kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye gharama nafuu za mawasiliano.

"Mifumo ya Tehama si salama kwa sababu Kuna maharamia ambao wanadukua taarifa za mtandaoni lengo kupoteza imani, fedha na sifa za serikali hivyo tutahakikisha tunalinda miundombinu ya mawasiliano dhidi ya hatari mbalimbali," alisema Dk Mwasaga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari alisema ni asilimia 30 pekee ya watalaamu walio kwenye sekta ya Tehama hivyo, idadi ya watalaamu ni ndogo na jitihada za lazima zinahitajika kukuza ujuzi kidigitali.

Alisema mapinduzi ya teknolojia yameongeza matumizi ya intaneti hivyo wanahitaji kuongeza usalama ili kukuza uchumi.

"Tunaomba bunifu zipewe kipaumbele kwani zina mchango mkubwa katika jamii na tunaamini Tehama itatoa fursa mbalimbali katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati," alisisitiza Dk Bakari.

Pia alisema wataendelea kuwezesha wasichana katika kutumia Tehama kujenga na kubuni mifumo na mitambo inayotumika katika shughuli mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad