HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 29, 2022

SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KUKUZA NA KULINDA HAKI ZA BINADAMU

 Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ina nia ya dhati ya kuendelea kuchukua hatua za kisera, kisheria na kiutawala kukuza na kulinda haki za binadamu na haki za watu.

Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati wa kikao cha 71 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kilichofanyika kwa njia ya mtandao huku kwa mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imetumika sambamba na lugha nyingine kama lugha ya kazi.

Dk.Ndumbaro amesema kuwa katika utekelezaji wa shughuli za Serikali yake, Rais amelipa kipaumbele suala la kulinda na kukuza haki za binadamu na watu.

” Serikali ilipata shilingi trilioni 1.3 za ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na janga la Covid-19 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mwaka 2021 ambazo zilitumika kununua dawa na maeneo ambayo yaliadhirika zaidi na janga hilo kama vituo vya afya, shule, mabweni kuchimba visima vya maji na kuimarisha programu za kuinua uchumi kwa kuzingatia makundi maalum hususani vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.”

Dk. Ndumbaro amesema katika kutekeleza wajibu wa kukuza na kulinda haki za watu, Serikali imekuwa ikiongozwa na misingi ya Utawala wa sheria na Utawala Bora.

Aidha amesema kuwa majadiliano na ushiriki wa wadau yamekuwa yakifanyika katika kukuza haki za kiraia na kisiasa na kusisitiza kuwa katika kukuza uhuru wa maoni na haki ya kupata taarifa, tozo za kusajili runinga za mitandao na magazeti na runinga za mitandao zilizokuwa zimefungwa kwa ukiukwaji wa kanuni za utangazaji zilifunguliwa.

” Serikali ina heshimu misingi ya demokrasia na uhuru wa watu, hivyo kumekuwa na jitihada za makusudi za kukuza haki za kiraia na za kisiasa.”amesema

Hata hivyo amesema kuwa hadhi za makundi maalumu hususani wanawake na wasichana pia zinaendelea kukuzwa na kulindwa.

” Serikali ilipitisha Waraka wa Elimu namba 2 wa Novemba 24 mwaka 2021 kuruhusu watoto walioachishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwamo ya kupata mimba waweze kurudi kwenye mfumo rasmi wa elimu baada ya kujifungua.”

Aidha, Dk Ndumbaro amesema Lugha ya Kiswahili imekuwa na mchango katika kuhakikisha nchi amani na utulivu mazingira ambayo yanawezesha wananchi kuendelea kunufaika na haki zao za msingi.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad