HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 6, 2022

Mwalimu Commercial bank yaja na huduma ya kusaidia wahanga wa Ada mashuleni na vyuoni

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko Mwalimu Commercial Bank, Leticia Ndongole akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam.Mshauri wa Mwalimu Commercial Bank katika masuala ya kutoa mikopo na huduma za fedha kwa Taasisi za Elimu, Issa Ngwegwe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Taasisi ya Institute of Heavy Equipment and Technology (IEHT),Mhandisi Edwin Godwin akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo cha Covenant Institute of Accountancy and Technology(CIAT), Godson Mkaro akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya ADA CHAP CHAP ambayo inalenga kuwasaidia wazazi/wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati uliofanyika leo Aprili 6,2022 Jijini Dar es Salaam.

KATIKA jitihada za kuboresha elimu nchini, Mwalimu Commercial benki, imezindua huduma ya Ada Chap chap  itakayosaidia wazazi na wanafunzi wanaokuwa wamekwama ulipaji wa ada kwa wakati kwa kuwapatia  mkopo.

iili kutimiza lengo hilo, benki hiyo meingia mikataba na wamiliki wa shule na vyuo mbalimbali nchini ili kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanafunzi.

Mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi wa ngazi ya elimu ya msingi, sekondari na  vyuo vikuu katika ngazi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko Letisya Ndongole, amesema kuwa mikopo hiyo itawanufaisha wazazi walioajiriwa kwenye taasisi za umma zile za binafsi, wajasiliamali pamoja na wanafunzi wanaojiendeleza wakiwa kazini.

“Huduma hii tumeiita  Ada Chap Chap, itakayoongeza thamani na kuwajengea uwezo wamiliki wa shule ili mikopo iwe na tija kwao”

Amesema kuwa wabia kwenye huduma hiyo ni pamoja na:-  Eag High School- Bagamoyo, City College of Health and Allied Sciences kampasi ya llala Goba (Mount Ukombozi), Covenant Institute of Accountancy and Technology -Kuras Covenant Financial Consultants kwa wanataaluma wa uhasibu yaani CPA na Institute Heavy Equipment and Technology - Kijitonyama.

Amesema benki hiyo inalenga kutoa huduma za kifedha kwenye taasisi za kielimu na wadau mbalimbali wa elimunm ili kuunga juhudi za serikali katika kuinua elimu pamoja na stadi za ujuzi kupitia vyuo mbalimbali


“Mwalimu Banki imelenga ikolojia ya elimu kwa wanafunzi kwenye vyuo vya elimu, Walimu, Shule, Taasisi za elimu, Wizara ya Elimu, TAMISEMI, Wafanyakazi wa Umma na Taasisi binafsi na wadau wote wanaotoa huduma kwenye sekta ya elimu (mfano watengeneza chaki,samani za mashuleni na vifaa vya shule”amesema Ndongole.

Ndongole amesema kuwa benki hiyo yenye vituo 9 sehemu mbalimbali nchini na matawi mawili jijini Dar es Salaam itatoa huduma hiyo ambayo pia itakuwa bima kwa mteja atakayepa ulemavu au kifo.

“Benki yetu mpaka sasa ina matawi mawili yaliyopo Dar es salaam(Samora na Mlimani) na tunavyo vituo vya huduma 9 (Morogoro, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Arusha, Rukwa, Kigoma,Mtwara na Arusha). Matarajio yetu ni kuwa na vituo hivo katika mikoa yote ifikapo mwaka 2025” amesema Ndongole.

Amesema kuwa banki hiyo imeandaa mkakati wa miaka mitano wenye lengo la kuboresha huduma zenye ubunifu kwa wateja wake “Moja ya maeneo yaliyopewa kipaumbele ni kuwa na bidhaa zinazolenga moja kwa moja mahitaji ya walimu, watumishi wa Umma, taasisi binafsi katika kujiinua kiuchumi na kuleta tija kwenye jamii”

Ndongole amesema kuwa benki hiyo imelenga  utoaji wa huduma za kibenki ambazo ni rahisi, salama na zinazopatikana popote na wakati wowote kwa njia za kidijitali ikiwa ni Pamoja na MwalimuMobile,MwalimuWakala na Mwalimu visacard.

Nae mmoja kati ya wabia hao, Shaban Mwanga kutoka Chuo cha Mkombozi cha Masuala ya Afya amesema huduma hiyo ya Ada Chap Chap ni ya umuhimu na  itasaidia wanafunzi wengi wanaoshindwa kuendelea na na masomo kwa sababu ya ada kuendelea na masomo yao kwa kupatiwa mkopo.

Amesema tatizo la ukosefu wa ada ni kubwa katika shule nyingi haswa vyuo vikuu na kupongeza benki hiyo ya Mwalimu kuliona hilo kwani kupitia Mwalimu Commercial Bank sasa suluhisho hilo litakuwa limepatikana.

Naye, Mshauri wa Mwalimu Commercial Bank katika masuala ya kutoa mikopo na huduma za fedha kwa Taasisi za Elimu Issa Ngwegwe amesema wameamua kusaidia benki hiyo kuhakikisha inajikita zaidi kuangalia sekta ya elimu kama sekta kwa ujumla hivyo wameanza na bidhaa hiyo ya Ada  Chap Chap lakini kuna mambo mengine yatataraji yanayyiohusiana na mikopo pamoja huduma zingine za kifedha katika Taasisi za Elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad