HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 12, 2022

MKAZI MOROGORO AHITIMISHA SPORTPESA BET BONANZA NA TSH. 15,888,000

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKAZI wa Lukobe, Morogoro, George Kimaro leo asubuhi ameibuka mshindi wa kufungia kampeni ya Bet Bonanza ya Sportpesa, baada ya kujishindia kitita kkikubwa zaidi cha shilingi 15,888,000 katika droo ya mwisho ya Bet Bonanza ambayo imefika tamati siku ya leo.

Katika droo hiyo ambayo pia imehusisha washindi wa droo ya shilingi milioni moja moja kwa kila mtandao, mchezaji Twaha Mustafa alishinda milioni moja kupitia mtandao wa Vodacom akitokea Arusha, mshindi mwingine Mohamed Mustafa wa Selous amepatikana kupitia Airtel na mshindi wa mwisho Thomas Uzuri wa Rukwa Sumbawanga amepatikana kupitia mtandao wa Halotel.

Droo hii ni sehemu ya promosheni ya Bet Bonanza ya Sportpesa, na pia ni muendelezo wa zawadi ambazo zilikuwa zinatolewa katika kipindi hiki cha ligi mbali zinazoendela kwa ushirikiano na kampuni za simu Vodacom, Airtel na Halotel.

Akizungumza baada ya droo iliyochezeshwa makao makuu ya Sportpesa, Jijini Dar-Es-Salaam, Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sportpesa Sabrina Msuya anasema leo imechezeshwa droo ya tano na ya mwisho katika kampeni ya Bet Bonanza, ambapo wateja wa Halotel, Airtel na Vodacom wamejishindia vitita hivi vya mamilioni ya shilingi kwa siku siku 35 mfululizo..

‘’Leo ndio imekuwa siku yetu ya mwisho ya kampeni yetu ya Bet Bonanza, muda mfupi uliopita imechezeshwa droo ambapo mteja wetu kupitia mtandao wa Vodacom George Kimaro (23) ambaye pia amemaliza chuo kikuu amejishindia Tsh 15,888,000, ambayo ndio ilikuwa zawadi kubwa kabisa na wengine watatu kutoka Airtel, Halotel na Vodacom.

Akitoa neno la pongezi kwa washindi George Kimaro Pamoja na Twaha Mustafa Meneja Biashara huduma ya Mpesa,Vodacom Kelvin Nyanda amewapongeza washindi wote wawili kwa ushindi wao na kuwataka watumie vizuri fedha hiyo kwa kuwa kipindi hiki ni cha sikukuu.

‘’Ninapenda kuwapa hongera washindi wetu wa leo, na pia napenda kuwashauri muendelee kucheza na Sportpesa kwa kutumia mtandao wetu wa Vodacom kupitia huduma ya Mpesa na pia mjitahidi kufanya matumizi mazuri hasa hasa kipindi hichi cha sikukuu ya Pasaka na mfungo wa Ramadhani.”

Akiwakilisha kutoka Halotel Afisa Masoko Roxana Kadio amempongeza Thomas Adam na pia amewapongeza washiriki wote walioshiriki kwa kutumia mtandao wa Halotel, na hata kama kuna ambao hawakushinda wasikate tamaa, kwani nafasi za ushindi zipo nyingi na wakijaaliwa watashirikiana na Sportpesa kwenye promosheni nyingine ambayo itajitokeza siku za usoni.

‘’Nawashukuru wale wote ambao tumekuwa pamoja kwa siku zote 35 za promosheni hii na pia nawapa hongera washindi wote walioshinda katika kipindi cha promosheni.

Naye mwakilishi kutoka Airtel Aggrey Charles alimpongeza Mohamed Mustafa na kumuhimiza kuendelea kucheza na SportPesa.

Akiwakilisha Bodi ya michezo ya kubahatisha ambao ndio walikuwa wasimamizi wa promosheni hii, Elibariki Sengasenga amewapongeza SportPesa kwa kuendesha promosheni hii kwa umahiri mkubwa Pamoja na washindi wote kwa ujumla kwa kushiriki na pia kuwataka kucheza kwa kuzingatia vigezo vya ushiriki katika mchezo huu.

‘’Ninapenda kuwaasa watanzania mcheze kwa kuzingatia vigezo na masharti ya promosheni mnazoshiriki na pia msisite kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi muda wowote ambao mtakuwa na Jambo mnalohisi linahitaji msaada wetu.

Ikumbukwe promosheni hii ilizinduliwa rasmi siku ya tarehe 8 Machi 2022, inajumuisha zawadi za shilingi elfu 20 kila siku, zawadi za milioni moja moja kwa washindi watatu kila wiki na zawadi ya milioni 15,888,000 siku ya kufunga kampeni.
Baadhi ya wawakilishi kutoka SportPesa Sabrina Msuya(kati), Airtel Money Aggrey Charles wa pili kushoto, Mpesa Frank Nyanda (wa pili) kulia pamoja na Halopesa Roxana Kadio(wa kwanza kulia) kwenye picha ya pamoja mmara baada ya kuchezesha droo ya kumtangaza mshindi wa shilingi 15,888,000 kwenye promosheni ya Bet Bonanza ambayo ilimalizika rasmi jana. Wa kwanza kushoto ni Frank Charles Gibebe mtangazaji kutoka SportPesa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad