Rais
wa Jamhuri Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Wakuu wa Mikoa katika
Halmashauri ambazo mfumo wa M-MAMA utatekelezwa, kutenga fedha
zitakazoongeza nguvu kwenye huduma ya mama na mtoto mchanga.
Rais
Samia amesema hayo leo wakati akizindua mfumo wa usafirishaji wa
dharura wa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) iliyoratibiwa na
kampuni ya simu ya Vodacom katika viwanja vya Chinangali.
Rais
Samia amesema lengo la mfumo huo ni kuhakikisha kuwa wakina mama zaidi
ya milioni moja ambao ni walengwa wanafikiwa na kunufaika na huduma hii
katika kipindi cha miaka mitano.
Aidha, Rais Samia amesema
tangu kuanza kwa majaribio ya mfumo wa M-MAMA katika Wilaya ya Sengerema
na mkoani Shinyanga mwaka 2013, wanawake na watoto 12,000
wameshahudumiwa na hivyo kusaidia kupunguza vifo vya kina mama
vinavyotokana na ukosefu wa usafiri.
Vile vile Rais Samia
ameitaka kampuni ya Vodacom kuufanya mfumo huo uwe endelevu na uwafikie
wananchi wengi na kutoa wito kwa kampuni zingine zilizopo nchini
kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Rais Samia amesema, pamoja na
jitihada zilizofanywa na Serikali, bado zipo changamoto ambazo
husababisha vifo vya mama na mtoto kabla au baada ya kujifungua kutokana
na kukosekana kwa mawasiliano ya haraka na usafiri wa uhakika wa
kumwahisha mama mjamzito kufika katika kituo cha afya.
Kwa
upande mwingine, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari kulinda taarifa binafsi za watumiaji wa M-MAMA ili
zikusanywe, kuchakatwa na kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni
zinazokubalika kimataifa.
ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Wednesday, April 6, 2022

MFUMO MPYA WA M-MAMA KUWANUFAISHA WANAWAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment