HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 2, 2022

HJFMRI waunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha chanjo ya Corona

 

Afisa kinga kutoka shirika hilo wa mkoa wa Mbeya Bi,Damali Lucas akieleza namna mradi wao unavyofanya kazi na kuisadia jamii katika maswala mbali mbali.
Baadhi ya wateja wakipata maelezo katika banda la Walter Reed
Dr.Cassian Nyandindi ni kamishna msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya akitoa wito kwa jamii kutoa taarifa juu watumiaji wa dawa ya kulevya ili waweze kusaidiwa.
Baadhi ya waelimishaji wakiwa katika banda kwa ajili ya kupokea wateja na kuelimisha juu maswala mbalimbali ikiwemo virusi vya ukimwi na madawa ya kulevya.

Na Amiri Kilagalila,Njombe
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ili kuhamasisha jamii kuelewa na kupokea chanjo ya Corona katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo,shirika lisilo la kiserikali la HJFMRI limetumia kikamilifu maonesho katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kwa kutoa elimu dhidi ya chanjo hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari katika banda lao lililopo katika uwanja huo utakapofanyika uzinduzi wa mbio za Mwenge kitaifa,Afisa kinga kutoka shirika hilo wa mkoa wa Mbeya Bi,Damali Lucas amesema jukumu lao kubwa nikuunga mkono serikali katika mapambano hayo.

“Kwa kushirikiana na mkoa wa Njombe tumekuja kusaidia kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha jamii kwenye maswala ya chanjo dhidi ya Uviko-19 kwa kuwa sisi ni miongoni mwa watu ambao tumechanja ili kujikinga na hata walengwa wote ambao tumekuja nao wote wamekwishachanja”alisema Damil Lucas

Aidha amesema shirika hilo kupitia Walter Reed wanatekeleza pia mradi unaohusika na kukinga maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutoa afua mbali mbali katika jamii ili kuendelea kukinga maambukizi ya virusi vya Ukimwi huku pia wakisaidia waraibu wa dawa za kulevya na kubainisha kuwa walengwa wao katika shirika hilo wapepatachanjo ya Corona ili kujikinga na maambukizi.

Boaz Tweve kutoka Rukwa na Sad Juma kutoka Mbeya ni miongoni mwa watu wanaofanya kazi na shirika hilo katika kuhamasisha na kushawishi wateja ikiwemo kupima virusi vya Ukimwi na kuanza kupata huduma za dawa wanasema wanatumia nafasi zao pia kuhamasisha chanjo ya Corona ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi.

Dr.Cassian Nyandindi ni kamishna msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti nan a kupambana na madawa ya kulevya amesema kupitia mbio za Mwenge wanatoa ujumbe na kuelemisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya yakiwemo madhara ya kiuchumi na afya lakini kwa mwaka huu wamekuwa wakizungumzia maswala ya Corona.

“Kupitia mbio za Mwenge kwa mwaka huu tunazungumzia swala zima la maambukizi ya Corona na kupokea chanjo,mapambano ni muhimu na ninapenda kuhamasisha umma kupambana dhidi ya Uviko-19 “Dr.Cassian Nyandindi ni kamishna msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti nan a kupambana na madawa ya kulevya

Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa juu ya watumiaji wa dawa za kulevya ili waweze kupata huduma.

Mbio za mwenge zinatarajiwa kuzinduliwa leo mkoani Njombe katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad