HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 23, 2022

Zitumieni Taarifa za Hali ya Hewa kwa maendeleo-Waziri Mbarawa

 


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Hali ya Hewa duniani leo Machi 23, 2022, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini, TMA Dkt Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Hali ya Hewa duniani leo Machi 23, 2022, jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI Nchini imetoa imetoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili kuimarisha mipango yao katika kufanya shughuli za maendeleo.

Wito huo umetolewa leo Machi 23, 2022, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya hali ya hewa Duniani.

Waziri Mbarawa ameeleza kuwa taarifa hizo zikitumika vizuri zinaweza kuwafanya wananchi kuelewa wakati gani sahihi wa kufanya shughuli Fulani za kimaendeleo bila kuathiriwa na mabadiriko ya hali yahewa.

“Nawahimiza wananchi mzitumie vyema taarifa hizi za hali ya hewa kwa ajili ya kupanga vyema shughuli zenu mbalimbali za maendeleo na katika kufanya maamuzi sahihi kwa ustawi na maendeleo endelevu ya nchi yetu”, amesema Mbarawa.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali imeweka jitihada za makusudi za kuboresha Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa taarifa hizo za uhakika.

“Serikali itaendelea kuwekeza katika uboreshaji wa vifaa vya hali ya hewa kuwa vya kisasa zaidi ambapo kwa kufanya hivyo inazingatia pia mikataba ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki unaozitaka nchi zote duniani kuachana na matumizi ya vifaa vinavyotumia zebaki”. Amesema

Mbarawa amesema kuwa TMA imefika kwenye kiwango cha kuridhisha ambapo imefikia kiwango cha asilimia 70 za kukubalika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini, (TMA), Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa Mamlaka hiyo imezidi kujiimarisha kwenye utoaji wa taarifa za hali ya hewa kwa lengo la kutoa tahadhari.

“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kupitia Serikali na wadau wengine imeendelea kuimarisha mfumo wa utaoji tahadhari kwa kuwashirikisha wadau nchini. Miongoni mwa juhudi hizo ni kufanya mafunzo na mikutano na wadau wakiwemo wanahabari na wafanya maamuzi”, amesema Dkt. Kijazi

Amesema kwa kuwa waandishi wa Habari husaidia kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wananchi na Mamlaka imekuwa ikiwapa mafunzo ya uelewa wa hali ya hewa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad