HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 27, 2022

ZAIDI YA MIL 41 ZATOLEWA KWA WAHANGA WALIOEZULIWA NYUMBA ZAO NA UPEPO


MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham aliyevaa shati la draft akiwa na unga na mabati kabla ya kuvikabidhi kwa wahanga ambapo ametoa bati 1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka mwezi wa tatu. 

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham wa pili kutoka kushoto akikabidhi msaada kwa unga kwa baadhi ya wahanga hao ambapo ametoa bati 1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka mwezi wa tatu.

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham akizungumza wakati wa halfa hiyo

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham ametoa bati 1190 mifuko ya Sembe 321 na Mbao za kuezekea nyumba kwaajili ya Kaya zilizoezuliwa nyumba zao na upepo mkali kuanzia mwezi wa kwanza 1 mpaka mwezi wa tatu.

Akizungumza katika mkutano na wananchi wa Tarafa ya mwaya Mbunge SALIM ALAUDIN HASHAM amesema amefanya hivyo kwa lengo la kuhakikisha kila familia inarejea kwenye mazingira ya awali waliyokuwa wanaishi ili waendeleze maisha kama zamani na waendelee kujitafutia kipato.

Hali hiyo inakuja baada ya ziara yake aliyoifanya wiki mbili zilizopita ya kukagua nyumba zilizoezuliwa na upepo na kujionea namna wananchi walivyopoteza makazi yao na vyakula kwa kipindi cha miezi mitatu.

Jumla ya Kaya 321 zilipata maafa hayo ya kuezuliwa paa za nyumba zao lakini mpaka sasa jumla ya Kaya 119 bado hazijarejea kwenye makazi yao kutokana na kushindwa kumudu gharama za kurekebisha makazi hayo.

Mbunge SALIM ametoa bati 10 kwa kila Kaya na mbao kwa Kaya 119 ambazo hazina makazi mpaka sasa na pia ametoa mfuko mmoja wa sembe kwa kila Kaya kwa jumla ya Kaya 321 ili kujikimu kwa chakula.

Aidha Mbunge SALIM ALAUDIN HASHAM amesema pia fedha hizo alizotumia ni kutoka mfukoni mwake na amefanya hivyo kwa lengo la kuona kila Mwananchi wa jimbo lake anapata ahueni ya Machungu hayo.

Jumla ya vijiji 15 vya wilaya ya Ulanga vilikumbwa na maafa ya kuezuliwa mapaa ya nyumba za wananchi kuanzia mwezi wa kwanza mpaka tatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad