HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 10, 2022

WAZIRI KIJAJI AELEZA MAFANIKIO MAKUBWA YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA NDANI YA MWAKA MMOJA

 



Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam wakati akieleza Mafanikio ya mwaka mmoja ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita.


MWAKA mmoja wa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan umeleta neema kubwa katika Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara hasa kwa kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji na ajira kwa watanzania  hali iliyopelekea mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji mbele ya waandishi wa habari wakati  akifafanua mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji  nchini hali iliyopelekea mapinduzi makubwa katika sekta ya uwekezaji wa viwanda na biashara.

 Waziri Kijaji amesema ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia, viwanda vipya vipatavyo 327 vimeanzishwa katika sehemu mbalimbali  nchini.

“ Namba hazidanganyi, Takwimu zinaonyesha katika mwaka mmoja wa uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, viwanda vipya 327 vimeanzishwa ambavyo vinajumuisha viwanda vikubwa, vya kati na vidogo." Amesema.

Aidha Waziri Kijaji amesema Wizara imekuwa ikipokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia yaliyolenga kuboresha mazingira ya wawekezaji ikiwemo kukomesha urasimu katika kuhudumia wawekezaji, kuimarisha mazingira ya biashara na kuondoa vikwazo visivyo vya lazima vya kibiashara baina ya Tanzania na nchi jirani.

Kuhusiana na idadi ya wawekezaji kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Machi, 2021 mpaka mwezi Februari 2022 Waziri Kijaji amesema, Serikali imefanikiwa kuvutia na kupitia kituo cha Uwekezaji  (TIC,) jumla ya miradi 294 yenye thamani ya shilingi Trilioni 118.75 imesajiliwa na itatoa ajira rasmi zaidi ya 62,000 kwa watanzania.

Akifafanua zaidi kuhusiana na manufaa kwa watanzania kupitia ajira hizo Waziri Kijaji amesema, nafasi za ajira hizo ni kubwa kuwahi kuandikishwa na kusajiliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania tangu kuanzishwa kwa Taifa tangu lipate Uhuru.

Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kudhibiti bei ya mafuta ya kupikia na sukari ambayo alisema haitabiriki kwa muda mrefu sasa, Waziri Kijaji alisema kwamba serikali imelipa uzito suala hilo, hivyo kuanzisha kongani za viwanda Dakawa, Morogoro ambapo maboresho makubwa yatafanyika kuanzia kwenye mbegu bora ili kuzalisha mafuta ya kutosha na kupata suluhisho la kudumu.

“ Mfumuko wa bei tulionao kwenye eneo la mafuta na sukari unasababishwa na sisi kutokujitosheleza na uzalishaji wetu wa ndani, hivi sasa tunategemea sukari na mafuta kutoka nje lakini tutakapoanza kuzalisha wenyewe hali hiyo itaisha”

Dk Kijaji ametoa wito kwa Watanzania kutoa ushirikiano wakati huu ambapo serikali inaanzisha kongani hizi, kujitokeza kutumia mbegu bora ili kutoa mazao yenye ubora ambapo pamoja na kongani za Dakawa kuna Mradi wa Mkualazi kwa ajili ya uzalisha wa sukari ambao upo kwenye maandalizi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad