DROO
ya wiki ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako
Vyako’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha matumizi ya
kadi badala ya pesa taslimu imefanyika jijini Dar es Salaam leo, ambapo
washindi 100 wamepatikana na hivyo kufanya jumla ya washindi
waliozawadiwa kufikia 950. Washindi hao 100 walijinyakulia kiasi cha Sh.
Mil. 10 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja), ambazo zinafanya zawadi za
pesa zilizotolewa hadi sasa kufikia Sh. Mil. 150 kati ya Sh. Mil. 240
zinazoshindaniwa.
Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa NMB,
Manfredy Kayala, alisema kumekuwa na mafanikio makubwa katika
uhamasishaji wa matumizi yasiyohusisha pesa taslimu na kuwataka wateja
kuendelea kutumia kadi zao na Vituo vya Mauzo (PoS), ili kujiongezea
nafasi ya kushinda katika fainali.
Droo hiyo iliyofanyika Makao
Makuu ya NMB, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, ilichezeshwa chini ya
uangalizi wa Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania
(GBT), Irene Kawili, ambaye aliwahakikishia wateja kuwa washindi
hupatikana kwa njia halali na kwamba vigezo na masharti vinazingatiwa.
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan Toufiq, amefanikiwa kuwa
miongoni mwa washindi 100 wa droo ya 10 ya msimu wa tatu wa Kampeni ya
‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga
kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu na alikiri kwamba
yeye ni mteja wa muda mrefu wa NMB, na kwamba kwa kipindi chote hicho
amekuwa ‘Balozi Mwema’ wa benki hiyo - miongoni mwa jamii inayomzunguka,
wakiwemo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anaoshirikiano nao.
Kujiweka kwenye nafasi ya kushinda droo ya
mwisho ya ‘Grand Finale’ ni rahisi, endelea kutumia NMB Mastercard
kufanya malipo mtandaoni, kwa QR code au POS na unaweza kujiweka kwenye
nafasi nzuri yakuingia kwenye draw.
Thursday, March 17, 2022

Washindi 100 wa droo ya 10 NMB MastaBata wapatikana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment