HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 8, 2022

WANANCHI WA GAIRO WAMUUNGA MKONO MHE SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUPANDA MITI

Mkuu wa wilaya ya Gairo Jabiri Makame akingoza zoezi la kupanda miti ikiwa ni sehemu ya Wilaya hiyo kutunza mazingira kwa kupanda miti
Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Gairo Robert Mwangosi ( kushoto) akifafanua jambo kuhusu upandaji miti.
Mkuu wa wilaya ya Gairo Jabiri Makame na baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakishiriki tukio la upandaji miti ikiwa ni mkakati wa Wilaya hiyo kuendelea kutunza Mazingira pamoja na uhifadhi.Miti hiyo inepandwa kutokana na ishi kati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gairo.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakishiriki tukio la upandaji miti ikiwa ni mkakati wa Wilaya hiyo kuendelea kutunza Mazingira pamoja na uhifadhi.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakishiriki tukio la upandaji miti ikiwa ni mkakati wa Wilaya hiyo kuendelea kutunza Mazingira pamoja na uhifadhi.
Wafanyakazi wa TFS akichukua mche wa mti kwa ajili ya kwenda kuipanda katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro
Wananchi wakina na Mkuu wa wilaya ya Gairo Jabiri Makame mkoani Morogoro wakielekea kwenye moja ya maeneo kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya Wilaya hiyo kutunza mazingira kwa kupanda miti
Mhifadhi misitu wilaya ya Gairo Morogoro Robert Mwangosi ameelezea jinsi wilaya hiyo ilivyojipanga kipindi hiki kua ndo kipindi kizuri kwaajili ya kupanda miti ambapo miti hiyo itaweza kufanya ufanisi mzuri katika kutengeneza hali ya hewa nzuri ambayo wanaitegemea.

Amesema wao kama wakazi wa wilaya ya gairo kutoka TFS kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya gairo wamejipanga vyema na wamekuja na kauli mbiu na mikakati madhubuti wa kuweza kukabiliana na hali ya jangwa na mikakati ya gairo yenye urithi wa kijani.

"Tumefanya mipango mbalimbali ya kujidhatiti ya upandaji miti ikiwa ni kuanzisha clubs, kuweka mbinu mbalimbali, kuwaunganisha wanafunzi kwa pamoja kuweza kupanda miti na kuweka miundo mbinu ya kufanya wanafunzi waweze kupenda mazingira na tumefanikisha kila mwanafunzi ana mti mmoja anaoweza kuusimamia toka ameingia shule hadi atakapo maliza" Amesema Robert G. Mwangosi.

Nae Mkuu wa wilaya ya Gairo Jabiri Makame amesema kampeni ya urithi wa kijani Gairo, ni kampeni ambayo inalenga kuibadilisha wilaya hiyo na kuwa ya kijani kwa kufanya harakati za upandaji wa miti na kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya suala zima la uhifadhi wa mazingira ili wilaya hiyo iweze kutoa mchango mkubwa katika kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika harakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad