KIKAO
kazi cha kimataifa cha wataalamu toka mashirika yasiyo ya kiserikali,
serikali na mashirika ya watu wenye ulemavu kinachohusu mbinu za
kukomesha unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wenye ulemavu kimeanza
kufanyika mjini Dodoma huku wataalamu waliobobea wakishawishi elimu
itakayowawezesha walemavu hao kujitegemea.
Aidha
kikao kazi hicho pia kinapitia mpango kazi wa mradi unaotekelezwa na
UNESCO na ILO Kupitia mradi unaofadhiliwa na United Nations Partnership
on the Rights of Persons with Disabilities (UNPRPD) wenye lengo la
kukomesha unyanyapaa na ubaguzi wa watu wenye ulemavu katika vyuo vya
ufundi na kazini.
Majadiliano
yalilenga zaidi katika kuhakikisha kwamba wanadamu wanavunja mzunguko
wa umaskini na kutengwa kwa watu wenye ulemavu.
Kongamano
hilo lililohusisha watu kutoka Tanzania, Msumbiji, Namibia na Zimbabwe
lilioanza Februari 28 hadi Machi 4 liliambiwa kwamba dunia ina watu
zaidi ya bilioni 1 wenye aina tofauti za ulemavu huku asilimia 80 ya
walemavu wote wanaishi katika nchi zinazoendelea.
Katika
mazungumzo ambayo mengine yalifanyika kwa njia ya video, ilielezwa na
Mtaalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(Unesco) anayeshughulikia masuala ya jamii na sayansi ya binadamu,
Ofisi ya Kanda Nairobi, David Ochieng Onyango, kuwa nchini Zimbabwe,
watu wenye ulemavu wanawakilisha asilimia 9 ya watu wote huku nchini
Tanzania watu milioni mbili wanaishi na ulemavu.
Kwa
mujibu wa mada iliyotolewa Onyango idadi hiyo ni sawa na asilimia 5.8
ya watu wote nchini, huku asilimia 50 yao hawawezi kumudu huduma za afya
huku wanawake wenye ulemavu wakiwa na uwezekano wa mara 2 au zaidi
kunyanyaswa kingono kuliko wanawake wasio na ulemavu.
Katika
kongamano hilo pamoja na washiriki kulielezwa kuwa miongoni mwa Malengo
7 ya SDGs yanarejelea kwa uwazi watu wenye ulemavu huku ikielezwa kuwa
suluhu ya maisha bora kwao ni kuwapatia masomo yanayohusiana na ufundi
kwa vitendo (TVET) na kupatikana kwa ajira.
"Watu
hawa wenye ulemavu wanaendelea kuachwa nyuma na hii imetokana na
masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na imani hasi za kitamaduni, kidini na
fikra potofu ambazo bado zipo miongoni mwa jamii," alisema Onyango.
Katika
kongamano hilo lilipata nafasi ya kuelimishwa kuhusu mradi wa Umoja wa
Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (UNPRPD) wenye lengo la kukomesha
unyanyapaa na ubaguzi na kuvunja mzunguko wa umaskini na kutengwa kwa
watu wenye ulemavu kwa mataifa ya Msumbiji, Namibia, Tanzania na
Zimbabwe.
Mradi huo
ulioshirikisha mashirika ya UNESCO na ILO wenye lengo la kusaidia nchi
hizo kuunda na kujaribu kwa pamoja mifumo na zana zinazoweza kusaidia
walemavu kwenye taasisi za Ufundi Stadi na Mafunzo (TVET), waajiri,
wafanyakazi na mashirika ya waajiri kuelewa kwa pamoja na kushughulikia
mifumo ya unyanyapaa na ubaguzi ambayo kuwepo kwa watu wenye ulemavu.
"Lengo
la kuboresha uwezo wa watu wenye ulemavu kupata programu za TVET na
kazi zenye staha kwa kubadilisha kanuni za kitamaduni, kijamii na kidini
zinazochochea unyanyapaa na ubaguzi." Alisema Onyango.
Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya UNESCO nchini, Bi Faith Shayo akisambaza nakala za mawasilisho ya mada wakati
wa kikao kazi cha kimataifa cha wataalamu kutoka mashirika yasiyo ya
kiserikali, Serikali na mashirika ya watu wenye ulemavu kwa lengo la
kukomesha unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wenye ulemavu kilichoratibiwa
na UNESCO na ILO kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa
Haki za Watu Wenye Ulemavu (UNPRPD) kinachoendelea mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali,
Serikali na mashirika ya watu wenye ulemavu walioshiriki kikao kazi
chenye lengo la kukomesha unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wenye ulemavu
kilichoratibiwa na UNESCO na ILO kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (UNPRPD) kinachoendelea
mjini Dodoma.Picha
ya pamoja ya wadau kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, Serikali na
mashirika ya watu wenye ulemavu walioshiriki kikao kazi chenye lengo la
kukomesha unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wenye ulemavu kilichoratibiwa
na UNESCO na ILO kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa
Haki za Watu Wenye Ulemavu (UNPRPD) kinachoendelea mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment