Na Khadija Kalili , Kibaha
Mkuu
 wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amemwagia sifa Rais wa Jamuhuri ya 
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameonyesha nafasi na
 uwezo wa Mwanamke duniani kutokana na uwezo wake mkubwa ameonyesha 
katika kuwajibika.
Amesema hayo wakati akizindua siku ya Wanawake
 duniani kimkoa katika viwanja vya Mailimoja mjini Kibaha na kuhudhuriwa
 na akinamama kutoka mkoa mzima wa Pwani.
Alisema hata wale ambao
 walikua na mashaka juu ya uongozi wa mwanamke kwa sasa kutokana na 
namna anavyoupiga mwingi hawana la kusema hivyo wanawake wote tembeeni 
kifua mbele kwani tunaye Kiongozi imara na madhubuti mwenye jinsia ya 
kike. 
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wadau wote 
wanaojishughulisha na masuala ya malezi ya watoto wa kike wakajifunze 
kwenye shirika lisilokuwa la kiserikali la Room to read ambalo 
linamuhudumia mtoto wa kike katika shule za msingi na sekondari za 
serikali kwa kutoa mafunzo ya stadi za maisha.
Alisema jinsi 
shirika hilo la Room to read linavyotoa ushauri, msaada wa vifaa na 
ushirikishwaji wa familia shule na jamii sambamba, elimu ya fedha na 
ujasiriamali na masuala ya usomaji na maktaba ni mbinu madhubuti katika 
kukusaidia moto wa kike na mwanamke kwa ujumla kujilinda hadi afikie 
malengo yake.
Aidha Alhaji Kunenge amewataka wanawake  
wajasiriamali kujituma zaidi Ili kuweza kujikomboa kiuchumi kwa kuleta 
maendeleo ndani ya familia na Taifa kwa ujumla.
RC Kunenge 
amesema haya  leo Machi mbili katika viwanja vya Maili Moja Wilayani 
Kibaha  alipokuwa akizindua  sherehe za kuelekea  siku ya Wanawake 
Duniani ambayo itaadhimishwa duniani kote ifikapo Machi nane ambapo kwa 
Mkoa wa Pwani maadhimisho haya yatafanyika kimkoa katika Halmashauri ya 
Chalinze huku kauli mbiu  ya mwaka huu inasema  'Haki na Usawa  kwa 
maendeleo Endelevu'.
Mkuu huyo wa Mkoa amewaahidi wajasiriamali  
hao kuwa atakutana nao Ili waweze kujadili masuala mbalimbali yanayo 
wahusu na siku hiyo atajaa nao kama Alhaji Kunenge huku akisisitiza kuwa
 wawe huru siku hiyo katika kuzungumza nae kwa kinaga ubaga.
"Tutakaa
 nawenzangu tuangalie namna ya kuweza kutoa mkopo wenye tija 
utakaomwezesha  mkopaji  kufanya jambo la maana pia tutawasaidia kuwapa 
mafunzo na miongozo Ili wakopaji  waweze kukopeshwa wakishafanikiwa 
waweze kukopeshwa wengine hili liko ndani ya uwezo wetu nitalijadili na 
Kamati yangu"alisemaKunenge.
Kila kikundi tutawafikia hakuna 
kundi au mtu atakayeachwa tutajitahidi tufungue fursa zaidi kwani njia 
ya kuwasaidia nyie ni kutoa fursa zaidi za kibiashara ,tuzingtie sheria 
na tutumie fursa.
"Tuhakikishe sisi sote tunashiriki katika sensa
 ya watu na makazi tujitokeze tushiriki vizuri na tupate chanjo za 
ugonjwa wa UVICO 19  takwimu zinaonyesha katika nchi yetu wale ambao 
hawajapata chanjo ndiyo wanaopata madhara zaidi" alisema Kunenge.
Katika
 sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali  wakiwemo Kamati ya 
Ulinzi na Usala ya Mkoa wa Pwani wengine ni pamoja na  Mwenyekiti wa 
Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani (UWT)Farida Mgomi ambaye alisema kuwa 
uzinduzi huu utaambatana na  kufanyika maonyesho ya bidhaa mbalimbali za
  wajasiriamali wa Wilaya Kibaha huku akitoa wito kwa wakazi wa Wilayani
 hapa kujitokeza katika kuwaunga mkono.
"Alisema kuwa baada ya 
uzinduzi huu Machi sita kutafanyika usiku Maalumu utakaofahamika kwa 
jina la Usiku wa wa Mwanamke wa Pwani ambapo kutafanyika mambo 
mbalimbali hasa kujua Mila na desturi za Mkoa waPwani' alisema 
Mwenyekiti huyo.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani Subira 
Mgalu ametoa pongezi kubwa kwa Wilaya na Mkoa kuandaa sherehe hizi 
ambazo kilele chake ni Machi nane .
Mkuu wa Wilaya Sara Msafiri 
alisema kuwa mwaka huu Wilaya imejipanga hivyo wataendelea  kutoa 
misaada mbalimbali ikiwemo kwenda kutembelea waginjwa katika Hospitali  
ya Ocean Road, gereza la Mkuza ambapo baadhi ya  wanawake kutokaWilayani
 hapa watakwenda kutoa misaada.
"Tumejipanga kuwajengea uwezo 
kina mama kwa kuwapa mafunzo Maalumu Ili waweze kupanda madaraja katika 
biashara  zao mwisho napenda kywashukuru wadhamini wetu ambao ni NMB, 
TRA, OSHA,TARURA,ROOM TO READ,TANESCO,DAWASA,TAKUKURU,.
Bendi ya 
muziki wa dansi ya Ruvu JKT ilitumbuiza sambamba na wasanii wengine kama
 Msaga Sumu, Yuda wote walinogesha uzinduzi huo 
Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ilianzishwa mwaka 1908 na kwa sasa inaadhimishwa  mwaka 101.
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment